20 June 2012

Dawa bandia ni tatizo la dunia nzima'



Na Heri Shaaban

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema kuwa suala la dawa bandia ni tatizo la Dunia nzima hivyo amewataka wananchi kushirikiana na serikali kiziba mianya ya uingizaji dawa bandia ili kulinda maisha ya Watanzania kwa ujumla.


Hayo yalisemwa Dar es Salaam hivi karibuni na Mkurugenzi wa TFDA Bw.Hiti Silo

Bw.Silo alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa la kidunia hivyo akuna budi kwa wadau,taasisi wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo pamoja na serikali kudhibiti njia za uingizaji wa bidhaa bandia.

"Kutokana na changamoto hizi TFDA imeweza kuunda vikosi kazi kwa ajili ya kusimamia udhibiti wa dawa bandia kila pembe ya nchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi kulinda mifumo ya njia hizo," alisema Bw.Silo.

Aliwaomba wananchi wanapopata taarifa za uingizaji wa dawa bandia, kutoa taarifa ngazi zinazohusika ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema kuwa mamlaka hiyo pia imeweza kuimarisha mipaka yote katika vituo vya forodha zinapoingia bidhaa kwa ajili ya ukaguzi kabla mzigo kurusiwa kuingia nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Hussein Mwinyi alikabidhi cheti kwa  Mamlaka ya chakula na Dawa  Tanzania TFDA na taasisi zingine zilizoshiriki madhimisho hayo ya siku ya famasia na kuwataka kutoa elimu ya kutosha  kwa wananchi ili wajuwe matumizi ya dawa bandia.



1 comment:

  1. HIVI TANZANIA TUMELOGWA NA NANI INAPOFIKIA RASILIMALIWATU TULIYONAYO INATHUBUTU KUTANGANGAZA HADHARANI KUWA MADAWA BANDIA HAWANA UWEZO WA KUDHIBITI BASI WATANZANIA WOTE TUTAAELEKEA KUZIMU MBONA WANAGOMA WAONGEZEWE POSHO WAKATI NI VIHIYO

    ReplyDelete