20 March 2012

Mkemia ashauri njia za kukabili utandawazi

Na Rabia Bakari
MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dkt. Daniel Matata amesema bado jitihada za ziada zinahitajika kuboresha mazingira ya sekta ya elimu hasa upande wa masomo ya sayansi ili kukabiliana na changamoto ya utandawazi.
Dkt. Matata aliyasema hayo juzi katika hafla fupi ya kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi 12 wa kidato cha nne na sita na shule zilizofanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Tuzo hizo zilitolewa na Chama cha Wakemia Tanzania (TCS) kwa kushirikiana na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

"Maabara na vifaa vyake hasa kwenye shule za serikali bado ni
changamoto kubwa hali inayopunguza hamasa kwa wanafunzi wengi kujikita
kusomea masomo ya sayansi," alisema Bw. Matata.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Bw. Charles Kitwanga, alisema Serikali imepanga kuongeza nguvu ya kuhakikisha masomo ya sayansi na kemia yanapewa msukumo ili kukabiliana na mabadiliko yanayochangiwa na utandawazi.

"Juhudi kubwa zinafanyika zikiwemo za kuboresha mazingira ya
kufundishia masomo ya sayansi, kuboresha maslahi y walimu, kujenga na nyumba na maabara zenye vifaa.

No comments:

Post a Comment