Na Mwajuma Juma, Mjini Magharibi
SERIKALI ya Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar imesema inakabiliwa na
changamoto za kutopata ushirikiano wa kutosha kutoka katika baadhi ya taasisi pindi zinapotekeleza majukumu yake mkoani humo.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa mkoa huo, Bw.Abdallah Mwinyi Khamis wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu, majukumu, mafanikio na changamoto katika utendaji wa mkoa huo.
Alisema, pamoja na kuwa ofisi yake ndiyo msimamizi mkuu wa mkoa huo, bado kuna baadhi ya watendaji wanashindwa kutoa taarifa kwa wakati hususani zile zinazohusiana na utekelezaji wa majukumu.
Alisema, hatua hiyo imekuwa ikisababisha watendaji wake wakiwemo masheha na wakuu wa wilaya na mkoa kutofahamu mambo yanayofanyika katika maeneo husika hivyo kuchochea migogoro ndani ya jamii.
“Changamoto kubwa inayoikabili Serikali ya mkoa ni kukosa ushirikiano wa kutosha kwa baadhi ya taasisi wakati wanapotekeleza majukumu yao
ndani ya mkoa bila ya kutujulisha au kutushirikisha," alisema
Hata hivyo alisema, mara nyingi taasisi hizo hufika kuwapa taarifa pale wanapokuwa tayari wamepatwa na matatizo ili kuwasaidia kuyapatia ufumbuzi hasa ujenzi wa miradi mbalimbali
No comments:
Post a Comment