Na Zena Mohamed
WATU wawili wamefariki jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti likiwemo la mfanya biashara Bw. Aloyce Asenga (27),kunywa sumu.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke,David Misime aliema tukio hilo lilitokea eneo la Tandika Mango ambapo Bw.Asenga alikutwa ndani ya chumba kimoja cha baa iitwayo Ngekewa akiwa hajitambui huku akitapika.
Alisema alikimbizwa katika Hospitali ya Temeke na kufariki baada ya muda, chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana na maiti imehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi.
Katika tukio jingine Bi. Sauda Abdu (35),alifariki baada ya kugongwa na gari akiwa kwenye bajaji.
Misime,alisema tukio hilo lilitokea barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Sabasaba ambapo gari lenye namba za usajiri T 170 BBD aina ya Toyota Rav 4 ikitokea Mbagala Mission kwenda Mbagala Kizuiani wakiwa ikiwa katika uelekeo mmoja iligonga pikipiki aina ya Bajaj yenye namba za usajiri T 843 ARA iliyokuwa ikiendeshwa na Bw.Mohamed Mkekenda (42),mkazi wa Mbagala.
Alisema ndani ya pikipiki hiyo kulikuwa na abiria ambaye alifariki papo hapo baada ya pikipiki aliyopanda kugongwa na dereva kupata majeraha na kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hata hivyo dereva wa gari hilo alikimbia na maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na jitihada za kumtafuta dereva wa gari hilo zinaendelea.
No comments:
Post a Comment