Na Mohamed Hamad, Arusha
WATANZANIA wameshauriwa kutumia madawa ya asili ambayo hayana kemikali yoyote
ili kukabiliana na maradhi mbalimbali yanayowasumbua hususani kisukari, shinikizo la damu pamoja na magonjwa ya zinaa.
Mwito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki mkoani Arusha na Dkt.Namdeo Shastri kutoka nchini India wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini humo mara baada ya kutaka kujua sababu za ongezeko la madawa ya asili kila kona ya jiji la Arusha.
Alisema, ongezeko hilo limetokana na idadi ya watu wenye matatizo mbalimbali ya magonjwa kusaka dawa baada ya kuona zile za hospilali haziwasaidii wakati mwingine kutokana na kukosekana kwa utaalamu wa kugundua ukubwa wa tatizo kabla ya tiba.
"Binafsi nina utaalamu wa muda mrefu niliopata toka Chuo cha Madawa ya Asili
kilichopo India ambapo pamoja na mambo mengine, niliweza kufika hata Mlima
Everest nchini India;
"Katika ziara hiyo niligundua madawa mengi yasiyo na kemikali, ambayo huwa yanawasaidia wagongwa mbalimbali isipokuwa kinachotakiwa ni utaalamu wa kutoa tiba hiyo na namna ya kutumia dawa wakati wa kuanza tiba,"alisisitiza Dkt. Shastri.
Alisema, yameibuka makundi ya watu wanaojiita waganga wa tiba za asili ambao wanatibu wagonjwa na hawajasomea wala hawana utaalamu wa kazi hizo.
"Na ukienda kwa kina utakuta shida ndizo zinazowasukuma kufanya kazi ili wapate kipato. Huko Ulaya hakuna mtu anayeweza kufanya kazi ya tiba kama hii bila kuwa na utaalamu hasa ikizingatiwa kuwa wanagusa maisha ya watu na wakati mwingine ukitokea uzembe maisha yao yanakuwa hatarini," alisema.
No comments:
Post a Comment