26 January 2012

SERIKALI imeshauliwa kutimiza malengo ya Milenia

Na Rehema Mohamed

SERIKALI imeshauliwa kutimiza malengo ya Milenia na mpango wa sera ya afya ili kupunguza vivyo vya watoto ambavyo vinavyoweza kuzuilika.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Eligius Lyamuya wakati akifungua semina ya wadau wa afya waliokuwa wakijadili hatua za awali za mradi wa kuhusisha jamii katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Mkoani Morogoro.

Prof. Lyamuya alisema asilimia 47 ya vifo vya watoto nchini hutokea mwezi mmoja baada ya kuzaliwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya watoto hao kuzaliwa wakiwa dhaifu.

Prof.Alisema kuwa baadhi ya wanawake hubeba mimba wakiwa na manonjwa ya kuambukiza kama Ukimwi hivyo wanaweza kuwaambukiza watoto wao kama hawajajijua mapema na kufuata sheria za afya.

"Utafiti huu utasaidia kuboresha afya ya Mama na Mtoto kwasababu vifo vingine husababushwa na matatizo ambayo wakati mwingine yanaweza kuzuilika, kama tutaweza kutimiza malengo ya milenia katika upande wa sekta ya afya tunaweza kupunguza vifo hivi "alisema Prof.Lyamuya.

Kwa upande wake Mkuu wa mradi huo Bw.ChristomLipingu alisema mradi huo utakuwa ukishirikisha jamii kuanzia ngazi ya chini ili waweze kuelewa masuala muhimu ya kuzingatia baada ya mtoto kuzaliwa ili kuimarisha afya yake pamoja na mama.

Bw.Lipingu alisema tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi nchini bado ni kubwa licha ya serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kujitahidi kulipunguza.

Bw.Lipingu alisema wakati mwingine matumizi ya njia ya uzazi wa mpango kwa wanawake baada ya kujifungua zinasaidia kupunguza vifo hivyo ingawa ni wanawake wachache wanaofanya hivyo.


No comments:

Post a Comment