Na Zahoro Mlanzi
KOCHA Mkuu wa mabingwa soka Tanzania Bara, Kostadin Papic ameutaka uongoza wa klabu
hiyo kumtafutia mechi moja ya kirafiki kabla hawajaumana na Zamaleki Februari, mwaka huu.
Katika kulifanikisha hilo, uongozi huo tayari imeshapata timu moja kongwe kutoka Afrika Kusini ambayo bado wanaendelea nayo kufanya mazungumzo ya mwisho.
Yanga itaumana na Zamaleki kati ya Februari 16,17 au 18 katika mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika, mechi itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na marudiano kati ya Machi 3, 4 au 5.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, Salum Rupia Papic aliomba kupewa apate mechi moja ya kimataifa na hilo litafanikiwa kwani tayari kuna timu imeonesha nia ya kukubali.
"Mechi hiyo itafanyika hapa Dar es Salaam wiki moja kabla hatujacheza na Zamaleki, nimepata taarifa kwamba kuna timu ya moja ya Afrika kusini ambayo ni kongwe imekubali kucheza na sisi," alisema Rupia.
Mbali na hilo, alizungumzia maandalizi yao ya ligi kuu ambapo alisema timu iliingia kambini rasmi jana kwa ajili ya mechi hizo na kwamba baada ya muda fulani watahama na kwenda nje ya jiji au ikiwezekana nje ya nchi.
Alisema baada ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi, timu yao ilipata majeruhi sita kitu ambacho kilirudisha nyuma programu ya mazoezi ya Papic na kumfanya aanza moja.
"Unajua kabla hatujaondoka, Papic alikataa kupeleka timu lakini ikachukuliwa tofauti na watu, sasa kile alichokisema kilikuwa cha msingi na sasa yupo katika kipindi cha kujenga timu kutokana na hali hiyo," alisema Rupia.
No comments:
Post a Comment