Na Queen Lema,
Arusha
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)mkoani Arusha umefanikiwa kukusanya sh. bilioni 16,745 kwa kipindi cha Julay hadi Desemba 2011 ambapo fedha hizo ni sawa na asilimia 92 ya lengo walilokusudia
Hayo yalisemwa na Meneja Kiongozi wa mfuko huo mkoani hapa Bw. Jackton Ochieng' alipokuwa akizukuhusu maendeleo ya mfuko huo.
Alisema kuwa mfuko huo umeweza kuandikisha wanachama 3582 ambapo ni sawa na asilimia 49.8 ambapo hilo ndilo lengo halisi na wamendikisha waajiri 72 ambapo ni sawa na asilimia 79 ya lengo hilo.
Bw. Ochieng' alisema kuwa mfuko huo umeweza kulipa mafao kwa wanachama wake 2416 ambapo kifedha wamelipwa sh. bilioni 4033.65.
Alisema changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni pamoja na watu kutojua dhana ya elimu ya mfuko wa jamii na hivyo kuwafanya kuwa waoga kujiunga na mfuko huo ambapo wamejitahidi kutoa elimu hiyo kwa waajiri 53.
No comments:
Post a Comment