25 January 2012

MOTO wateketeza Nyumba na Baa katika maeneo tofauti jijini

Zourha Malisa

MOTO wateketeza Nyumba na Baa katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam ikiwemo Bw. Anna Lusiba (52),mkazi wa Mikocheni B,  moto kuzuka ghafla.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela,  alisema tukio hilo limetokea eneo la Mikocheni B, kwenye  nyumba ya  vyumba 3 yenye plot namba 227.

Alisema moto huo uliozuka ghafla uliteketeza nyumba hiyo pamoja na mali zilizokuwemo ndani ikiwemo bastola na risasi 50 ambazo ni mali ya mpangaji wake, ambaye ni mfanyabiashara Bw. Michael Kufrey (62), raia wa Ufaransa.

"Moto ulizimwa na kikosi cha zimamoto na hakuna madhara zaidi kwa binadamu na upelelezi unaendelea,"alisema kamanda Kenyela.

Katika eneo la Kiwalani Relini katika baa iitwayo Gombero mali ya Afisa Uhamiaji   Bw. Hussein Mayeto (50), mkazi wa Buza Kipera.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Ilala, Faustine Shilogile, alisema tukio hilo lilitokea juzi katika ukumbi wa baa hiyo uliojengwa kwa makuti moto uliwaka ghafla na kuteketeza ukumbi huo pamoja na viti na meza.

Alisema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na hakuna madhara kwa binadamu na thamani ya vitu hivyo bado haijafahamika.

Wakati huo huo gari yenye namba za usajili T 774 ATY aina ya Honda ilikamatwa ikiwa na viroba 13 vya dawa za kulevya aina ya bangi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke,David Misime, alisema gari hilo ilikamatwa eneo la Kongowe na askari wa doria walipoitilia mashaka gari hiyo na kuisimamisha kwa ajili ya kuipekuwa ndipo walipokuta dawa hizo.

Alisema baada ya gari kusimamishwa dereva wa gari hilo aliruka na kukimbia, gari hilo pamoja na viroba vya dawa hizo vimehifadhiwa katika kituo cha polisi Mbagala na jitihada za kumtafuta dereva huyo zinaendelea.



    

No comments:

Post a Comment