Grace Ndossa na Rehema Maigala
*Serikali yaahidi kuwalipa walimu Januari 2012
SIKU chache baada ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutangaza mgomo uliopangwa kuanza Januari 2012, Serikali imeahidi kulipa anza kulipa sh. bilioni 30.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Selestine Gesimba, alisema tayari tume iliyoundwa na Serikali, imefanya uhakiki ili kujiridhisha na madai hayo.
“Awali CWT ilesema fedha wanazoidai Serikali ni sh. bilioni 49.6 lakini tume tuliyounda imebaini madai haya yanafikia sh. bilioni 52,” alisema Bw. Gesimba.
Alisema tume hiyo ilikamilisha uhakiki huo Desemba 2 mwaka huu ambapo Januari 2012, Serikali italipa malimbikizo ya mishahara sh. bilioni 30 na madai mengine ni sh. bilioni 22 ambazo zimeanza kulipwa Desemba mwaka huu.
Bw. Gesimba alisema kuwa, sh. bilioni 45 ni madai kutoka katika halmashauri ambapo sh. bilioni saba zinadaiwa na taasisi zinazohusika na elimu.
Waalimu kueni na tahadhari za Serikali zinazoambatanishwana masharti kama ya uhakiki n.k. Ahadi kama hizo ni za kununua muda tu. Jiulizeni ni kwa nini Serikali haikuwa imefanya huo uhakiki. Mtakuja kuambiwa baadhiyenu mnataka kuiibiaserikali kwa madai ya uongo. Ili mradi kuzushwe kisa cha kuchelewesha malipo yenu. Mtaweza kupigwa goli la kisigino! Kumbukeni ya CAG alivyowacharurura mlipotaka kugoma.
ReplyDeleteCWT simamani imara. Kama mtaghilibiwa, amueni kuwashawishi waalimu watumie silaha yao kubwa ya KURA huko mbeleni. Mkiwatishia nayo watawalipa haraka sana.