07 December 2011

Mvua yaleta madhara makubwa Ruvuma

Na Cresensia Kapinga,Songea.

MVUA zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara makubwa kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma baada nyumba 20
kuezuliwa ikiwemo chumba kimoja cha darasa katika Shule ya Msingi Azimio.

Kuezeliwa kwa nyumba hizo ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa wiki ikiambatana na Radi na upepo mkali katika kijiji cha Azimio Wilaya  ya Tunduru mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Bw. Michael Kamuhanda, alisema licha ya nyumba hizo pia mvua hizo ziliharibu vitu mbali mbali ambavyo thamani yake bado haijafahamika.

Hata hivyo alisema hakuna mwananchi yeyote aliyeumia wala kufariki kutokana na maara hayo ya mvua na kwamba idara husika inafanya tathimini ili kujuwa thamani halisi ya hasara ilitokana na mvua hizo.

 Kamanda Kamuhanda alisema kuwa kufuatia maafa hayo watu waliopata maafa hayo hawana chakula hivyo wameomba watu na mashirika ya umma na binafsi kuwasaidia chakula kutokana na vyakula vyao kuharibiwa na mvua hiyo.

No comments:

Post a Comment