*Aponda mfumo timu za taifa
Na Speciroza Joseph
BAADA ya kutoka kapa katika michuano ya Kombe la Chalenji, Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa amevunja ukimya kwa
kusema mfumo wa timu za Taifa nchini ndio chanzo cha kufanya vibaya katika michuano ya kimataifa.
Mkwasa alitoa kauli hiyo baada ya kumalizika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ambapo timu yake ilifungwa 1-0 na Sudan kukosa nafasi ya tatu, ya pili ikachukuliwa na Rwanda na Uganda wakatwaa ubingwa wa michuano hiyo ilioshirikisha timu za mataifa 12.
Alisema Kili Stars na Zanzibar wataendelea kuona mashindano hayo magumu kwa kuwa zote zinaunda timu moja hivyo, linapokuja suala la kutenganisha timu hizo zinakuwa hazina nguvu ya kutoa kiushindani kama zilivyo timu nyingine.
“Timu zetu huwa ni za mpito zinaandaliwa kwa ajili ya michuano hii tu tofauti na timu zingine kama Uganda na Rwanda ambazo wapo kwa muda mrefu wakifanya mazoezi hali ambao imezijenga timu hizo na kuzifanya ziwe imara kipindi chote cha mashindano”.alisema Mkwassa.
Aliongeza kuwa, kutenganisha timu ya taifa kunaathari kuu moja ambayo wachezaji watakaoongezwa katika timu hizo na itawachukua muda mrefu kutengeneza timu imara.
Akizungumzia mashindano ya mwaka huu, alisema timu yake imecheza kadri ya uwezo na kukubali kuwa walizidiwa na timu walizokutana nazo na kuongeza kuwa mashindano yalikuwa magumu na yenye ushindani zaidi.
Mkwasa alisema aliwatumia wachezaji wapya na vijana katika timu yake ikiwa ni sehemu ya kuwapa uzoefu wachezaji hao ili kuweza kulitumikia taifa miaka ijayo.
Kocha huyo mzawa, alisema tatizo la mashabiki kuwa tofauti na timu kwa kiasi kikubwa kumechangia timu hiyo kufanya vibaya kwa kuwa anaamini mchango wa mashabiki uwanjani ni moja ya sehemu ya mafanikio kwa timu husika.
Makocha hongereni kwa kukubali zigo la Taifa ukweli timu yoyote duniani haiwezi kuandaliwa kwa wiki mbili ikawa bora na pia wachezaji muwache kuchagua majina hao baadhi yao wana kiburi iwe isiwe wanajijuwa mtawachaguwa tu mbona kuna vijana wazuri wengi tu
ReplyDeletekunatim zimejikusanya siku mbili tu hauna sera nenda tu kwenyetim yako ya madem uliowazoea hata ungepewa mwaka uiandae hakunajipya hapo mnang'ania wazalendo wapewe tim ndio mmepewa na mmeshindwa kila siku hukosi sababu mkwasa angalia kiwango kilichoonyeshwa na tim yako ndio ujue ww ni kocha wa madem tu ndio saizi yako kama ulijua muda ni mfupi uliopewa kuianda kwa nn usikatae?na ulianza kwa mkwara wa nguvu za chadema? sikubaliani nawe na wala sikukubali kuwa kocha wa tim ya wanaume ya taifa
ReplyDeleteuwezo mdogo tu. hakuna lolote. hiyo timu ta taifa yenye mchanganyiko bara na visiwani inafanya nini? kila siku kufungwa tu. tatizo mpira wetu upo mdomoni. ungetueleza haya mapema kabla hata ya mashindano, mlijinasibu sana hapa kabla ya mashindano.kumbe mlikuwa nasifia timu mzuri kwa kuangalia mazoezi yenu. kwenda kwenye game hakuna kitu. mi nilikuwa nashangaa sana unajisifu kwa kufanya mazoezi tu, tayari timu mzuri.
ReplyDeleteHebu tumuulize Mkwasa Zimbabwe na malawi wameitwa dakika za mwishoni lakini wamefanya kitu kinacho onekana.Tanzania tumezoea mpira wa mdomoni.Alafu hawa ndio wanaolalamika hawapewi nafasi za kuonyesha vipaji vyao vya ukocha.Je huu ukocha mmeusomea?au kwa sababu ya kuchezea Simba na Yanga muda mrefu.Tff wanatakiwa kujuwa ya kwamba kocha anatakiwa asomee ukocha na kuwa na mbinu za kisasa za kufundisha wachezaji pamoja na kuwasoma wachezaji wake vizuri.Tumeona Sudan wameleta timu ya vijana ambao baadae watakuwa hazina kubwa ya taifa lao,Sisi tumekazana na vijeba wetu ambao hata nidhamu hawana.
ReplyDeleteSio kocha wala timu, kiwango cha mpira wa Tanzania ni kidogo. Cha muhimu ni kutafuta wakala wa kupeleka wachezaji nje ya nchi. Hakuna timu ya taifa ya nchi yoyote wanaokuta kwa mwezi mzima labda wakati wa World Cup. Watu wakiwa wanacheza soka ya kulipwa Ulaya, wanajua nini cha kufanya. Wakikutana kwa wiki mbili wanajaribu formation na few tricks basi. Lakini hiyo timu yenu inayotoka kufundishwa na Kibadeni na mwingine anatoka kufundishwa na Njohore. Leo wakutane wacheze soka nzuri ni ndoto ambayo haiwezi kutimia. Angania chini zote za Afrika wanaocheza soka nzuri wanatoka Ulaya, wakirudi nyumbani wanatumia skills walizozipata huko.
ReplyDeletempira hauchezwi kwa kurundika lawama nani alaumiwe bali fundi n mwenye ubunifu wa kufundisha na uongozi wenye kutimiza majukumu yote na kuwajibika! Tutawalaumu sana makocha ilihali tukiuacha ukweli ukiendekea kupeperusha bango la "UBABAISHAJI' Ndani ya TFF!
ReplyDelete