Mkuu wa wilaya ya Moshi, Bw. Musa Samizi (aliyesimama), akizungumza na msafara ulioshuka kutoka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro (hawapo pichani) jana. wengine toka kushoto ni Mkurugenzi wa Zara Tours, Bi Zaynab Ansell, Meneja wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Tawi la Arusha, Bw. Willy Lyimo, Kulia Bw. Madaraka Nyerere. |
Hongera sana Ndugu Madaraka Nyerere kwa kushiriki kupanda Mlima Kilimanjaro pamoja na wakimbiza mwenge na wote warioshiriki katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru. Kazi uliyoifanya ni ishara ya uzalendo wa hali ya juu kwa taifa letu na watu wake. Pasina shaka umeyatimiza maneno ya Baba wa Taifa ya kuuwasha mwenge na kuuweka katika Mlima Kilimanjaro ili umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete upendo pale penye chuki na haki pale penye dhuluma juu ya hayo ulete tumaini pale penye kukata tamaa. Tanzania ya sasa inahitaji uzalendo mliouonyesha.
ReplyDelete