Na Pendo Mtibuche, Dodoma
JINAMIZI la kutaka kumtimua Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, limechukua sura mpya baada ya
Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama hicho, Bw. Moses Machari, kusema kuwa kama harakati za kumuondoa zitafanikiwa, wanaoendesha harakati hizo za usaliti dhidi ya mwenyekiti wao wakifanikiwa yuko tayari kujiuzulu ubunge na kuwa mwanaharakati.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, mbunge huyo alisema mgogoro huo uliodumu sasa ndani ya chama chao unatokana na uroho wa madaraka kwa baadhi ya viongozi wanaotaka nafasi ya Bw. Mbatia na si vinginevyo.
Alisema hivi sasa imefikia wakati baadhi ya viongozi kutumia fedha zao kurubuni baadhi ya viongozi wa chama hicho ili wapite mikoani kufanya shinikizo la kumkataa Bw. Mbatia na kutoa tuhuma ambazo si sahihi.
"Jambo hili nalipinga kwa nguvu zote, si sahihi baadhi ya viongozi ndani ya chama chetu tukaanza kusalitiana kwa kutumia fedha walizonazo kutaka kuondoa viongozi kwa malengo yao binafsi, hili likitokea mimi nitajiuzulu ubunge na kuwa mwanaharakati wa kawaida tu," alisema mbunge huyo.
Alisema chanzo cha vurugu zote ndani ya chama hicho ni kutokana na viongozi kuhusika kupigania madaraka kwa masilahi yao binafsi na kutaka kukivuruga.
Aliwatuhumu viongozi hao aliowataja kuwa ni wasaliti kwa Bw. Mbatia na kueleza kuwa baadhi ya madai yao si sahihi ikiwemo ya matumizi mabaya ya ruzuku ya chama hicho ya sh. milioni 130 kwa mwezi na kwamba ni uzushi na hoja ya kukosa kugombea na kukosa ubunge kwa mwenyekiti huyo haina msingi kwa kuwa hata yeye aliwahi kukosa.
Alisema chama hicho kinapata ruzuku ya sh.milioni 12 kwa mwezi na siyo milioni 130 kama inavyodaiwa na wabaya wake hao wanaonyemelea nafasi yake na kuwataka wanaotaka kuthibitisha hicho kwenda katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Bw. John Tendwa.
Alisema watu hao ndiyo wanaoeneza uvumi kuwa Bw. Mbatia ni wakala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka wajitokeze hadharani kuthibitisha hayo madai ili watumie katiba ya chama chao kukomesha hayo kama yapo.
Akizungumzia vikao vilivyoendeshwa na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Dodoma ulioripotiwa kuvunjika na baadhi ya vyombo vya habari baada ya hoja hiyo ya Bw. Mbatia kuingizwa alisema viongozi hao wanatumiwa na baadhi ya kundi hilo linalompinga Bw. Mbatia kutekeleza hayo wanayotaka.
Alisema kutokana na hali hiyo wanawaomba wanachama wao kusimama imara na kulaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wanaopita huku na kule kueneza uongo dhidi ya mwenyekiti wao.
Kwa upande wake Kamishna wa chama hicho Mkoa wa Dodoma, Bw. Mohamed Kabutari, ambaye ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kupewa fedha kwa ajili ya kueneza kile kinachodaiwa kuwa ni maovu ya mwenyekiti wao kwa lengo la kumkataa alisema yeye anamkataa Bw. Mbatia kwa madai kuwa ni azimio.
Alisema yeye kama Mjumbe wa Halmashauri ya chama hicho taifa, katika mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika Dar es Salaam Novemba 5, mwaka huu kilichohusisha wajumbe 28 wote waliazimia kutokuwa na imani na mwenyekiti wao hivyo suala hilo si kwamba yeye kama kamishna wa chama hicho Mkoa wa Dodoma anamkataa.
Akizungumzia madai ya Bw. Machari kuwa wapo viongozi na wanachama wanaopewa fedha ili kumkataa Bw. Mbatia alisema hayo ni maneno ya kitoto na kukanusha mpango wowote wa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mwenyekiti kama inavyodaiwa kuwa wapo baadhi ya watu majina tunayo.
Alisema hata kama mbunge huyo atajiuzulu nafasi yake ya ubunge, chama hicho hakiwezi kuyumba na kudai kuwa yeye hana ugomvi wowote na baadhi ya viongozi wenzake wa chama hicho mkoani Dodoma.
Alisema katika kikao chao walichokifanya mjini Dodoma kwa kuhusisha wenyeviti wa majimbo sita ya Mkoa wa Dodoma yaani Kibakwe, Bahi, Mtera, Kondoa Kusini, Kondoa Kaskazini na Kongwa walizungumzia mambo mbalimbali ya chama chao.Hata hivyo kikao hicho kilidaiwa kuvunjika baada ya hoja ya kutaka wamkatae Bw. Mbatia kuwasilishwa.
Machali acha ujinga na discussions za kisiasa zisizo na maana na tija concentrate kutuletea developments Kasulu. Unatumia too much time and energy kwenye siasa feki badala ya kujihusicha na maendeleo ya jimboni kwako. Acha kabisa hiyo trend, utakosa ubunge soon if u dont change.
ReplyDeleteujinga mtupu
ReplyDeleteHizo ndizo siasa za Kiafrika kutaka madaraka ili watafune pesa na sio kusaidia wananchi,subirini 2015 muone Kasheshe,msifikiri itakuwa ccm peke yake ni vyama vyote vitaingia kwenye misukoko mikubwa ya kugombea madaraka (mlo)
ReplyDeleteMachali tulikupigania sana mpaka hatukulala kwa aili yako badala ya kuzungumzia maslahi ya wanajimbo wako umekalia siasa uchwala. Ukijiuzulu na kwetu usije kwani utakuwa umetusaliti.
ReplyDelete