*Wanaghushi nyaraka kuwezesha upatikanaji dhamana
*Wadaiwa kushirikisha makarani, waendesha mashtaka
Na Gabriel Moses
MAHAKAMA za Jiji la Dar es Salaam zimevamiwa na kundi kubwa la vishoka wanaodaiwa kughushi nyaraka mbalimbali za serikali na kukwamisha upatikanaji wa haki za
wananchi wanaohitaji huduma za chombo hicho muhimu nchini.
Baadhi ya nyaraka zinazotengenezwa na kundi hilo ni pamoja na barua za kudhamini washitakiwa pamoja na kurubini ndugu za watuhumiwa kutoa kiasi cha fedha ili kuwawezesha kupata dhama za watuhumiwa.
Kundi hilo inadaiwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa mahakama wasio waaminifu wakiwemo makarani, waendesha mashitaka na mahakimu kufanikisha malengo yao huku baadhi ya watu wakikosa haki zao za msingi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwepo kwa kundi hilo katika karibu za Mkoa wa Dar es Slaam huku wakiranda randa eneo hilo kuwavizia watu wanaokabiliwa na kesi hasa wanaotafuta wadhamini.
Idadi kubwa ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamekuwa wakiingizwa 'mjini' kwa kile wanachodaiwa kusaka wadhamini hao kwa kutumia nguvu za fedha ili waweze kupata dhamana.
Mmoja wa wananchi aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kindondoni jina linahifadhiwa alisema kundi hilo liliwai kumwibia sh. 100,000 kwa lengo la kupata dhamana.
"Sasa kuna makundi hayo na yanatoweka na fedha nyingi za wananchi hawa wanyonge,ndio maana kuna malalamiko mengi kutokana na watu waliokimbiwa na vishoka baada ya kuwapa fedha nyingi.
Miongoni mwa mahakama zinazodaiwa kuwa na vinara wa makundi hayo kuwa ni pamoja na Ilala, Kinondoni, Temeke na Kisutu.
Vishoka hao uomba kati ya sh.100,000 hadi 500,000 kulingana na uzito wa kesi na kutoa hati feki za nyumba pamoja na barua za dhamana kutokana na masharti yaliyowekwa na mahakama husika.
Akizungumzia hali hiyo mmoja wa hakimu wa mahakama ya Ilala alikiri kuwepo kwa watu na kuongeza kuwa tayari wamtumishi wa mahakama wamepwa onyo kali kuwa makini na watu hao na kutoshiriki vitendo hivyo.
Ilielezwa kuwa mapema mwaka huu mahakama hiyo iliwatia hatiani watumishi wawili wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) na Mamlaka ya Maji safi na Mkoa wa Dar es Slaam (DAWASCO) kwa kosa la kumwekea dhamana raia wa China ambaye si ndugu yao kisha kutoroka licha ya kuwa na barua halali.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Kisutu, Ilvin Mgeta, alisema tangu aanze kazi mahakamani hapo hakuwahi kusikia malalamiko ya aina hiyo.
Alisema mhakama hiyo ipo makini katika kuchunguza hati na barua za wadhamini ili kutotoa nafasi kwa watu kama hao.
"Sijawahi kupata malalamiko hayo sijui kwa wenzangu waliotangulia, wewe uliwahi kusikia malalamiko hayo, basi kama yapo mimi sijawahi kupata taarifa hizo," alisema hakimu huyo.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni, Kwey Rusema, alisema awali kulikuwa na kundi hilo la watu lakini kwa sasa halipo kutokana na operesheni ya kuwasaka na kuwakamata.
"Awali hata baadhi ya makarani na waendesha mashitaka wa polisi walikuwa wakidaiwa kushirikiana na watu wa aina hiyo, hata hivyo nilitoa onyo kali dhidi ya watu hao na kwa sasa hali ni shwari
"Nina uhakika kwa sasa hakuna makundi hayo jambo la msingi hata kama wewe unawafahamu watu si mbaya ukatusaidia ili sheria ichukue mkondo wake, wanakwamisha kesi za msingi kutokana na watuhumiwa kukimbia pindi wanapopata dhamana," alisema.
Mmoja wa Mahakimu kutokana mahakama ya Temeke, alikiri kuwapo kwa vishoka hao licha ya kupungua kutokana na baadhi yao kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
"Mwanzoni hali haikuwa shwari kabisa, malalamiko yalikuwa mengi, sasa unaweza kusema pametulia kutokana na agizo lililopo la kuwataka watumishi kuachana na vishoka hao na atakayebainika kufukuzwa kazi mara moja," alisema.
Hiyo ni danganya toto,nenda mahakama za Mwanza utashuhudia hata hakimu anajihusisha na matapeli hao.
ReplyDelete