08 November 2011

Gaga atesa tuzo la MTV

BELFAST,  Ireland Kaskazini

MWANAMUZIKI Lady Gaga, juzi alitamba katika sherehe za utoaji wa tuzo za muziki za MTV Ulaya,  zilizotolewa Odyssey Arena, Belfast, kwa kupata tuzo nne.

Kwa mujibu wa  Shirika la Utangazji la Uingereza  (BBC),  nyota huyo wa muziki wa pop kutoka Marekani alipata tuzo ya Wimbo Bora, Video Bora, Msanii Bora wa Kike na Kipenzi cha Mashabiki.

Katika sherehe hizo, alitumbuiza na kama kawaida yake, alivaa mavazi mbalimbali, ikiwemo gauni la rangi ya fedha kubwa na kofia kubwa kama dishi la setelaiti.

Mwanamuziki kinda Justin Bieber na mwimbaji wa R&B, Bruno Mars nao walipata tuzo mbili kila mmoja .

Baada ya kutumbuiza, Lady Gaga  alisema amefurahishwa kwa kupata tuzo hizo.

Alisema hakutarajia mambo yangekuwa rahisi kwake na kwamba,  amekuwa akipambana ili kutoka chini kwenda juu.

Mchezaji sinema David Hasselhoff  alipata wakati mgumu kushikana mikono na msanii huyo bora wa kike mwenye umri wa miaka 25.

"Nilikuwa nikijaribu kushikana naye mkono, lakini nikaishia kugusa tuzo,"  alisema na kuongeza .

Orodha ya washindi wa tuzo la MTV EMAs 2011 ni kama ifuatavyo; Best Female, Lady Gaga, Best Male na Justin Bieber, Best Pop.

 Justin Bieber, Best Song, Lady Gaga, 'Born This Way', Best Rock, Linkin Park, Global Icon, Queen, Best Video, Lady Gaga, 'Born This Way', Biggest Fans, Lady Gaga,

Tuzo ya Best Live Act - Katy Perry, Best Alternative, Thirty Seconds To Mars, Best Hip Hop, Eminem, Best World Stage, Thirty Seconds To Mars, Best Push, Bruno Mars na Best New, Bruno Mars.

No comments:

Post a Comment