08 November 2011

Burns amtwanga Katsidis

WEMBLEY, Uingereza

RICKY Burns, juzi aliibuka na  ushindi dhidi ya Michael Katsidis katika pambano lililofanyika Uwanja wa Wembley Arena.

Burns alikwenda katika pambano hilo huku akiwa hapewi nafasi kubwa ya kushinda, baada ya kupoteza ubingwa wake wa dunia uzani wa super-feather na kisha kuingia katika light.

Kwa mujibu wa The Sun, bondia huyo alicheza vizuri na kuweza kutwaa taji la WBO .
\
Akiwa na furaha, bondia huyo kutoka Scotiland alisema: " Siamini. Nimewathibitishia watu waliokuwa wakinifikiria vibaya na niko juu ya mawingu.

"Bila ya kujalisha ninapigana na nani, nitajitolea kwa asilimia 110 na kujua nitashinda. Ngumi yangu ya jab ilikuwa ngao na nitaendelea kusonga.

"Ninafikiri niliwathibitishia watu hawakuwa sahihi, kulikuwa na mazungumzo mengi yaliyosambaa kuhusu Michael.

"Nile wakati nimekuwa nikisema kunapikuwa na mpiganaji yeyote mzuri mbele yangu, nitakuwa mzuri zaidi.

Burns mwenye 28,  alionekana kuwa na hakika katika mechi yake ya kwanza ya uzaji wa light.

Kidogo ilikuwa ni kama kitu cha kushitua wakati majaji watatu walipompatilia alama nyingi za kumpa ushindi baada ya kumalizika kwa raundi 12.

Burns,  ambaye sasa ana rekodi ya kushinda mapambano 33, kati ya 35 , alisema: "Ninalichukulia kwa namna moja kila pambano na ndivyo ninavyoona.

"Siongopi kupigwa kwa kuwa, kupoteza pambano si mwisho wa dunia, kwa hiyo ninataa kupigana na kila mmoja.

No comments:

Post a Comment