18 July 2011

Wenger amtaka Mancini kujiheshimu

HANGZHOU, China

KOCHA Arsene Wenger amemlalamikia kocha wa Manchester City, Roberto Mancini kwa kukosa heshima baada ya kusema hadharani kuwa anamtaka Samir Nasri.Wenger
yuko na timu yake China ambapo juzi ilicheza dhidi ya Hangzhou Greentown na kutoka sare ya bao 1-1, alikasirishwa na maoni ya  Mancini,  ambaye alisema kuwa anataka kumsaini kiungo mwenye miaka 23 Nasri ambaye amekataa kusaini mkataba mwingine bila ya kuboresha zaidi mshahara wake


Kwa mujibu wa Daily Maily, Mancini alifanya mahojiano ya televisheni mwishoni mwa wiki akieleza nia yake ya kutaka kumsaini mchezaji wa Ufaransa kabla ya mwisho wa mwezi na kocha wa Gunners  tayari amesema anataka kumbakiza mchezaji huyo pamoja na Cesc Fabregas  ambaye pia anatakiwa na Barcelona.

" Ninafikiri kuwa maoni hayaruhusiwi, yanapingana sheria za soka na anatakiwa kuelezwa," alisema Wenger.

"Sijui ni kitu gani kinatakiwa kufanywa. Situmii muda wangu kuanza kuogopa kile kinachosemwa na watu wengine, kwa kuwa tunaweza mtazamo katika mchezo wetu.

"Tunachotaka ni heshima na hatutoi maelezo kama haya kwa wachezaji wenye mikataba katika klabu. Hakuonesha heshima?Siwezi kusema vinginevyo. Maoni yake ni kinyume kabisa, lakini siwezi kuyapa umuhimu huo."

Karibuni Wenger aliilaumu Man City kwa kukubali udhamini wa pauni milioni 400 na kampuni ambayo ina ukaribu na wamiliki wake wa Abu Dhabi ambapo inapingana na sheria ya inayokataza kutumia fedha nyingi zaidi.

Mancini anataka kumsaini  Nasri anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30 ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Msimu uliopita kocha wa Arsenal, Wenger alifanya bishara na City kwa kuwauza wachezaji Kolo Toure, Emmanuel Adebayor na mwaka huu Gael Clichy.

No comments:

Post a Comment