18 July 2011

Miss Kinondoni kuoneshana vipaji leo

Na Mwandishi Wetu

WAREMBO waanaowania taji la Redd's Miss Kinondoni 2011, leo wanatarajia kuchuana vikali katika kinyang'anyiro cha vipaji 'Miss Talent' kitakachofanyika katika hoteli ya
Giraffe ocean View, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa shindano hilo, Omari Yusuf alisema warembo hao watachuana kuwania taji hilo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na fainali ya mashindano hayo.

"Kesho (leo) warembo wanaowania taji la Redd's Miss Kinondoni watapanda jukwaani kuwania taji la vipaji 'Miss Talent' na kwamba warembo wote wapo katika ari ya kushindana,"alisema Yusuf.

Alisema warembo watakaowania taji hilo la Miss Talent ni Fatma Pongwe, Winnie Gerald, Mariam Almas, Stella Premsing, Hamisa Hassan na Stela Mbuge.

Wengine ni Husna Maulid, FElister Filip, Stella Moris, Naomi Jones, Pamela Gordian, Renalda Apojei na Sabrina Sabrina Abdalah.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment