22 July 2011

Samuel Sitta apigwa 'pini' Dar

Na Anneth Kagenda

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta, ametakiwa kuacha mara moja tabia yake ya kuikashfu ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utekelezaji
wake kwa kuwa kufanya hivyo ni kuupotosha umma.

Kadhalika, Bw. Sitta ametakiwa kutoitisha mkutano wowote kwa wakazi wa Dar es Salaam hadi apate barua kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete na endapo hatapata aendelee kufanya katika mikoa mingine.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Bw. John Guninita alipofanya ziara katika Kata ya Mbezi na Kata mpya ya Msigani kuzungumza na viongozi wa chama hicho ambapo alisema kuwa pamoja na kutoruhusiwa kufanya mkutano huo, pia Bw. Sitta aache kuleta maslahi ya kunyimwa uspika kwenye chama.

Kauli ya Bw. Guninita inashabihiana na iliyotolewa juzi na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki aliyewazuia Bw. Sitta na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye kufanya mkutano jimboni mwake kuhubiri siasa zao za kuvuana magamba.

Bw. Guninita alisema kuwa hivi karibuni Bw. Sitta alikaririwa kwenye mkutano wake mkoani Mbeya akisema maneno ya 'kuikashfu ilani ya CCM' huku akisema kuwa Tanzania siyo nchi maskini kama inavyoelezeka, eti serikali haijatekeleza ilani na kusema kuwa kufanya hivyo anakuwa hakitendei haki chama hicho huku akiupotosha umma wa Watanzania kwa maneno yake hayo.

"Viongozi wa namna hii tusiwavumilie hata kidogo mtu kama Waziri Sitta hawezi kukaa kwenye mkutano kama ule na kusema maneno ya namna hiyo ikizingatiwa yeye alikuwa waziri tangu enzi za hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini pia utaratibu wetu ni kwamba mtu akikerwa na jambo fulani anakaa kwenye vikao na kuzungumza hivyo kuzungumza maneno hayo ndiko kunakusababisha chama kishindwe kwenye chaguzi.

"Isiwe kuwa ni hasira ya kuondolewa uspika ndiyo inayo mpelekea kusema hivyo kwani kilichofanyika bungeni ni kutaka 50 kwa 50 kwamba kipindi hiki aongoze mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Anne Makinda, hivyo aache kuleta nongwa kwenye chama, ninawaomba ndugu zangu wana CCM mpuuze Waziri Sitta kwani inaonekana ana mipango yake mingine anayoijua mwenyewe," alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema kuwa maneno ya Waziri huyo ni ya kukibomoa chama kwani hajatumwa na Katibu Mkuu Taifa, Bw. Wilson Mukama wala Rais Kikwete na kwamba viongozi hao hawawezi kumtuma maneno ya kubomoa serikali yao na kuuyumbisha umma kama alivyofanya.

Bw. Guninita alisema kuwa ikiwa watu wa namna hiyo wataendelea kuachwa upo uwezekano mkubwa wa kukipoteza Chama ifikapo uchaguzi wa 2014/2015 na kusema kuwa hali hiyo inasababisha upinzani kuendelea kujipanga ukiwa na matumaini kuwa wakipata urais basi watakuwa wamemaliza kila kitu.

"Huyu Bw. Sitta mimi nashindwa kumuelewa anapokaa barabarani na kusema adharani kuwa Ilani haijatekelezeka anataka tukienda viongozi tupigwe mawe kwa sababu kufanya hivyo ni kutaka wananchi watuone hatufanyi kazi yoyote ya kuwaletea maendeleo kwani CCM ndicho chama kinachotawala anaposema nchi siyo maskini anamaanisha kwamba viongozi hawawajibiki ipasavyo," alihoji.

Akizungumzia kuhusu kujivua gamba alisema kuwa watu wamekuwa wakipotosha kuhusu neno hilo na kusema kuwa maana ya kujivua gamba ni kubadilisha tabia na wala siyo kufukuzana na kusema kuwa kufukuzana ni kukibomoa chama hicho.

"Nimekuwa nikienda sehemu mbalimbali utawasikia wanachama wakisema mvue gamba huyo katibu, hatuwezi kwenda hivyo kinachotakiwa ni kukaa kwenye vikao, kuelezana, kuelimishana na kusema ukweli mtu akionekana hakubaliani na yale anayotakiwa kufanya hatua zitachukuliwa dhidi yake lakini siyo kwamba mtu anajivua gamba anafukuzwa hata Rais Kikwete hapendi tabia hii," alisema.

Aliwataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanawajibika ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wananchi na kujua matatizo waliyonayo na kusema kuwa kufanya hivyo ndio utakuwa muarobaini wa kukifanya chama hicho kiweze kushika dora.

24 comments:

  1. Badala ya kujadili mambo ya maendeleo na zaidi utatuzi wa masuala magumu yanayotukabili, viongozi mnakaa kurumbana juu ya jambo kama hili. Cha msingi wajibikeni wakuu.
    Otherwise upinzania utaendelea kujizolea misifa.

    ReplyDelete
  2. Hii ni taarifa tu kwa mkubwa Guni, watanzania wa leo hawahitaji kuambiwa na Sita juu ya mapungufu yaliyopo katika mfumo wa uongozi uliopo. Watanzania wanajua, watanzania wanaona, watanzania wameelimika sana. Ninavyofaham mimi SITA NI MKOMAVU KISIASA NA NIMPAMBANAJI WA KWELI. Mpinge kwa hoja na sio ubabe wa madaraka ya mkoa, ukishampinga kaa chini upime hoja zake na zako uone zipi zinamashiko kwa umma! Ni hayo tu kaka.

    Mtanzania aliye gizani

    ReplyDelete
  3. Sisi wananchi tunampenda na tunamsikiliza Mh. Sitta vizuri kabisa. Yeye ni mtanzania na ana haki na uhuru wa kuongea jambo lolote ambalo anafikiri ni jema kwa mstakabali wa taifa. Katika vita hii tuko na Sitta na he will win softly!

    ReplyDelete
  4. Yaone yanaanza vita yenyewe kwa yenyewe. Hizo ndizo nyufa zinazoleta mpasuko kwenye chama hiki chenye mafisadi lukuki na ambacho kinakumbatia ufisadi kwa dhati. Enyi wapinzani, kuweni na mshikamano na kuwangoa hawa. Wametuchosha.

    ReplyDelete
  5. Bw Guninita,
    inaonekana mkiambiwa kwenye vikao hamtekelezi wala kusikiliza ndio maana Mh Six ameamua kuwaambia watu ambao watamsikiliza. Ushauri wa bure, anayekuambia kweli anakupenda,badala ya kumlaumu chukua nafasi hii kurekebisha kasoro ambazo Mh Six anazinadi mwishowe atakuwa hana cha kuzungumza.

    ReplyDelete
  6. Mr 6, ninakupenda kwa kuwa wewe ni mtanzania halisi. ninakupenda kwa kuwa inawezekana kabisa wewe ndiwe kwa sasa umeshika kifimbo cha mwalimu kuchapa chapa hawa wahuni ili kurudisha nidhamu katika nchi yetu na pia uwajibikaji....nakupenda kwa kuwa unaelewa WAJIBU WAKO KATIKA JAMII!! Mungu akuzidishie maisha! - Tanzania bila viongozi wahuni INAWEZEKANA!!!

    ReplyDelete
  7. HIZI SIASA ZA KUTAFUTA UMAARUFU NA KUJIFAGILIA KWA AJIRI YA KINYANGANYIRO CHA URAIS MWAKA 2012 NDIO CHANZO ZA SIASA ZA MAJI TAKA.
    HAZIJENGI KABISA NDIO KWANZA ZINAKIDIDIMIZA CHAMA HIVYO NASHAURI WANACCM HAYA MAKUNDI YOTE TUYAPIGE CHINI TUJE NA MTIZAMO MPYA WA KUWAACHIA VIJANA HAPA NAMSHAURI MH RAISI WEMBE UWE ULE ULE SASA NI ZAMU YA WANAWAKE HAWA WANAUME WOTE NI WANAFIKI ACHIA KITI SASA MWANANMKE ROZO MIGILO HII NDIPO KOMESHA YA MAKUNDI YOTE NA KAMPENI ZITAKWENDA VIZURI NA MAKUNDI YATABAKI NA AIBU.

    ReplyDelete
  8. Ni Ukweli usiopingika kwamba Tanzania sio nchi masikini ila viongozi wake ndio wana fikra masikini. Hii inajidhihirisha wazi kwa bwana Gunninita badala ya kujadili hoja ya msingi jinsi ya kuondoa umasiki kwa wananchi anamzuia Sitta kusema ukweli, na anamzui kwa manufaa ya nani wakati nchi ni yetu sote na kamwe sio ya viongozi tuu. Fungueni macho sisi wana CCM tunawaangalia tuu jinsi mlivyo na ubinafsi lakini siku ikifika msishangae tukawapigia wapinzani kura kwasababu tangu uhuru mnakula wenyewe tuu wananchi hawafaidiki na chochote, sera na ilani za chama zinaishia kuwa porojo tuu.

    ReplyDelete
  9. Wananchi waliosoma na wanofikir mara zote watamuunga mkono sita kwa sababu yuko against na sera ya CCM ya kulindana hata kama yanayofanywa na kiongozi ni mabaya. Mh. 6 usiogope simama katika kutetea wanyonge. wakikufukuza unahamia chadema halaf waone moto wake 2015.

    ReplyDelete
  10. Nakunukuu we tahaira Gininita!Bw. Guninita alisema kuwa hivi karibuni Bw. Sitta alikaririwa kwenye mkutano wake mkoani Mbeya akisema maneno ya 'kuikashfu ilani ya CCM' huku akisema kuwa Tanzania siyo nchi maskini kama inavyoelezeka, eti serikali haijatekeleza ilani!!!!!. Je ni uongo kuwa rais hasemi haya? Haya yanamkera sana Bwn 6 ndio maana ameamua kusema na hii sio kwaajili ya wananchi tuu ila ni ujumbe kwenu nyie waujumu nchi! Mwalimu alisema kuwa! Mpinzani wa kweli atatoka CCM na hii ni wazi kabisa. Je we Guninita ulitaka 6 aseme nini ktk mikutano yake? Hiyo hoja mweleze mkeo tena na watoto wako wasisikie kwani ni upuuzi mtupu!

    ReplyDelete
  11. acha hizo Guninita unajifanya unaipenda sana CCM mbona uliikimbia na kwenda upinzani?ama kweli nyani haoni kundule yaani hii leo umeshasahau duh...kazi ipo kweli kweli mgosi

    ReplyDelete
  12. Hi watanzania! Amuakeni kuzuia mipango ya wakina Guninita kuweka mafisadi kwenye uchaguzi ujao. Ni nani asiyejua Guninita Rostam na Lowasa ni pete na chanda. Guninita unakiwa kujenga hoja ndugu yangu. Kwa kutumia madaraka umejidharirisha sana ndugu kuna social change kubwa Tanzania kwa sasa na wewe huna habari. Sitta anaiokoa CCM kwa taarifa yako. Kwani watu wanajua ndani ya CCM kuna watu makini kama Sitta. Watu wanamheshimu sana Sitta kwani amejijengea heshima kubwa miongoni wa watanzania. Na wanamsikiliza ukibisha itisha mkutano wewe na Sitta uone watu watakwenda kwa nani. Ni ukweli usiopingika kwamba CCM walimtoa Sitta kiubabe kwenye uspika. Na mimi nimojawapo niliyeuzika sana. Kwani alikuwa ni spika wa viwango. Hoja ya Gender haikuwa na mshiko hata kidogo. Timiza wajibu wako Guninita achana na Mh Sitta

    ReplyDelete
  13. SITTA anapiga kampeni ya kupata urais mwaka 2015 kupitia CCJ.

    SITTA anataka kuiua CCM na arudi kuimarisha CCJ.

    Hata MBOWE alimshangaa sita. Alimshauri rais avunvje kabineti yake kwa kuwa mawaziri wake wanapingana. Inakuwaje SITTA kwenda Mbeya na kumkandya Ngeleja? Kwanini hakufanya hivo katika kabineti? Ni MNAFIKI

    ReplyDelete
  14. SITTA ana hasira ya kukosa uspika. Sasa anataka kuwa rais. Hatufai.

    Anaefaa ni Dr. Slaa. Achaneni na SITTA.Huyo ni CCJ

    Akija CHADEMA tumkatae. atakiwa chama kwa njaa zake za vyeo

    ReplyDelete
  15. Sita anafanya kazi za Wilson Mkama. Ni kampeni ya urais 2015 au ni hasira za kukosa uspika? Huo ni unafiki mkubwa. sisi tunaona kua ccm haielewani. hivo haitufai

    Wachangiaji wengine ni mbumbumbu. Ni nani aliyesema kua Lowasa bado ana nia ya urais?

    Hata kama anayo. ni nani aliesema kuwa ccm itampitisha?

    ReplyDelete
  16. HEKOHEKO SIX WAPASHE HAO MAMBUMBUMBU HAWAJUI KUWA TANZANIA NI NCHI TAJIRI KULIKO NCHI ZOTE AFRICA MASHARIKI SASA GUNINITA JAMANI HUWEZI KUSHINDANA NA MSOMI KAMA HUYO SIX NI ENGINE KUBWA NA KWA TAARIFA YENU MSIJE KMAKAJARIBU KUMUUZI SIX AKIONDOKA TU CCM KWA KHERI MTUMIENI HUYO MZEE VIZURI AKINUSURU CHAMA NA SIO KUKURUPUKA KAMA NDEGE KWENYE KICHANJA CHAKEKUWENI MAKINIMCCM

    ReplyDelete
  17. HELLO! Mr guninita very sorry for your IGNORANCE About your country the country is so rich so unajaribu kuupotosha umma ukuamini kuwa nchi hii ni maskini waakati sio kweli SIX WEMBE ULEULE BABA WACHANE HAO WANAFIKI WASIOJUA NCHI YAO TUKO NYUMA YAKO VIJANA TUNASUBIRI JEMBE LETU HUKU BABA ULIME HATA KTK MWAMBA PASUA WEWE WAACHE WAJIDANGANYE WATAONA WALETE HABARI ZA WANAWAKE 2015 WATAONA MOTOWAKE HAO CCM

    ReplyDelete
  18. Mawazo finyu,mawazo finyu,mawazo finyu!Wenye akili wanajulikana:Little mind discuss people,Middle mind discuss events BUT Great minds discuss IDEAS.Achana na Guninita na Sitta.Choose the best.Don't Bring Changes but suggest Changes.Ciao!

    ReplyDelete
  19. Siwezi kutoa maoni yangu juu ya maneno yaliyoelezwa na Guninita, huyu darasa la saba kihiyo huwezi kuwa kiongozi kwenye karne ya 21 John jivue gamba.

    ReplyDelete
  20. huyu guninita, mshamba na ni maskini wa mawazo.hao ndo mafisadi. naona tuanzishe sheria mpya tuwabane na kupigwa risasi kwa wahujumu uchumi.

    ReplyDelete
  21. Mheshimiwa Guninita unapoteza muda wako kumpinga mtu kama Sitta, anasikilizwa zaidi na wananchi kuliko wewe, hoja zake ni nzito na zinamantiki kuliko zako, watanzania wanaelewa vizuri sana kuwa hoja ya kuwa na Spika mwanamke safari hii ilikuwa ni kumwondoa Sitta na si kuwajali wanawake. Kama kweli CCM na serikali yake wangekuwa wanajali matatizo ya wananchi na wangekuwa wanajua kuwa matatizo hayo yanapaswa kujadiriwa kwenye vikao, basi serikali ingekuwa ilishayafanyia kazi siku nyingi mapendekezo ya tume ya akina Mwakyembe kwa serikali yaliyotolewa Bungeni wakati wa Uspika wa Mheshimiwa Sitta. Kumpinga Sitta ni kumwongezea umaarufu, ni afadhali kukaa kimya!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  22. Mwananchi amekandamizwa mpaka amekata tamaa ikifika wakati wa uchaguzi anapata kofia na t-shirt kwani na kilo ya mchele. Hii ni kejeli kwa mtanzania . Naomba watanzania tuamke na kuanza kamapeni kuanzia sasa tuwang'oe hawa matumbo makubwa tumeonewa kiasi cha kutosha.

    ReplyDelete
  23. Kidumu chama Tawala.

    ReplyDelete
  24. Waziri Sitta ni miongoni mwa viongozi makini ambao wananchi walikuwa wakiwaheshimu na mimi mwenyewe nikiwemo.Jambo ambalo limenikwaza nikaanza kujiuliza maswali ni jinsi anavyotoa matamshi yake na hasa pale alipoanza kuwaponda wapinzani kuwa ni wanafiki.Sitta huyu huyu tena kaanza kuwapinga wenzake wa chama tawala.Je sasa yuko upande gani? Upinzani anaponda Chama tawala anaponda.Namshauri kama amezeeka kisiasa apumzike asije jivunjia heshima

    ReplyDelete