22 July 2011

Hamad Rashid amshtaki Nape bungeni

*Ni kwa kumkejeli Maalim Seif

Na Gladness Mboma, Dodoma

MBUNGE wa Wawi (CUF), Bw. Hamad Rashid amemshtaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye kwa
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kwa kumkejeli Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Bw. Maalim Seif Sharif Hamad na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alisema hivi karibuni Bw. Nape alikaririwa katika vyombo vya habari akimkejeli Bw. Maalim Seif wakati Rais Jakaya Kikwete alipongeza juhudi hizo zilizofikiwa na viongozi hao wa Zanzibar.

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua serikali inatoa kauli gani kuhusu suala hilo.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alieleza kushangazwa na mbunge huyo kutomweleza suala hilo, kwani ni rafiki yake sana na wamekuwa wakikutana mara nkwa mara.

Hata hivyo, alisema kama kuna Watanzania wanakejeli hatua hiyo ni upungufu wa watu wenyewe na kwamba Mtanzania yoyote aliyekuwa akifuatilia siasa za Zanzibar, hawezi kukejeli hatua hiyo.

“Hatua iliyofikiwa ni mfano wa kuigwa, kama watu hao (wanaokejeli) ni viongozi wa serikali ninong’oneze,” alisema Pinda na ndipo mbunge huyo alipomtaja Nape na Bw. Mwigulu Mchemba na kusema kuwa wamekaririwa kwenye magazeti.

Hata hivyo, Bw. Pinda alipotajiwa majina hayo alionekana kugwaya na kusema kama suala hilo lipo kwenye magazeti si la kutiliwa maanani.

“Mimi naamini sana runinga kwa sababu namuona mtu mwenyewe, lakini kwenye magezeti inategemea ni gazeti gani. Magazeti mengine yana ajenda zao,” alisema na kuongeza kuwa atalifuatilia suala hilo.

17 comments:

  1. Ukweli hawa wenzetu kina Nape tangu wapewe hizo nyadhifa wamejisahau. Kauli zao wanazozitoa kwenye majukwaa sio nzuri kwa wana-CCM wenye upendo wa dhati na chama. Nasema hivyo kwa sababu zinawagawa wanachama wetu. Kwa sababu hata wao huko walikotokea mpaka kupewa hizo nyadhifa wakifuatiliwa kwa kina sio wasafi 100% sasa hakuna sababu ya kunyoosheana vidole. Sidhani kama ndio kazi waliyopewa ya kukashifu wenzao. Kazi yao ni kukijenga chama upya kujaribu kupunguza mapungufu. Sasa wenzetu hawa tangu wapewe hivyo vyeo wamefurahia kwa ajili ya kulipiza visasi tu na si vinginevyo. Haswa huyu NAPE viongozi wa chama wamuangalie sana kwani inawezekana kabisa mpasuko ndani ya chama ukaongezeka kutokana na kauli za hawa.

    ReplyDelete
  2. Mi binafsi nashangaa, aliyempa Nape uongozi nae hana akili. Kama alivyosema Rostam Aziz, ameamua kuachana na siasa uchwara za CCM. Siasa uchwara huwa zinatoka kwa wanasiasa uchwara na wanasiasa uchwara huwa ni products za chama uchwara. CCM ni chama uchwara

    ReplyDelete
  3. NAPE NI MFYATUKAJI,ATAWAHARIBIA CCM

    ReplyDelete
  4. LAKINIU PANDE WA PILI WA SHILINGI NI KWELI ALIVYO WAKEJELI NAPE,MAALIMUCUF NA VIONGOZI WENZAKE,SASA WANAKULAKUKU KWA MRIJA WAMELEMAZWA SANA NA MUAFAKA.VIONGOZI WANASHINDWA HATA KUWATETEA WANAONYANYASWA,KISA MUAFAKA.MFANO,SUALA WA MBUNGE MAGDALENA SAKAYA KUKAMATWA KINYUME NA UTARATIBU,KUNYANYASWA KWA KUSWEKWA RUMANDE CHUMBA KIMOJA NA VIJANA WA KIUME KWA WIKI TATU KULE TABORA,HALIJASEMEWA NA WABUNGE WAKE WALA VIONGOZI WA KITAIFA,LICHA YA HARAKATI ZA KUTAKA KUANDAMANA AMBAZO AWALI WALIKUWA WAKIWAPINGA WAPIZAN WENZAO- CHADEMA, ZILIZOONESHWA NA JULIUS MTATIRO AMBAYE BAADAE INADAIWA BAADAE ALIPIGWA STOP NA VIONGOZI WA JUU WA CUF. CUF WAJUE KUWA SASA WANAKULA WALICHOPANDA

    ReplyDelete
  5. NAPE NI MWANASIASA WA CCM NA SHARIF IN MWANASIASA WA CUF, HIVI NI VYAMA VIWILI PINZANI KATIKA MEDANI ZA SIASA. SITEGEMEI NAPE KAMA MWANASIASA AMSIFU SHARIF KAMA MWANASIASA WA UPINZANI. MUAFAKA HAUFANYI CCM KUWA CUF WALA CUF KUWA CCM. HIVI VINABAKI KUWA VYAMA TOFAUTI VYENYE ITIKATI TOFAUTI NA NI PINZANI. MAALIMU SASA ANAMEREMETA TU NDANI SHANGINGI LA SERIKALI AMESAHAU WALALA HOI ALIOKUWA ANAWATETEA. NDIO MJUE HAWA CHADEMA MNAOWASHABIKIA KUWA ETI NI WATETEZI WA WANYOKE NI DANGANYA TOTO TU, WANATAFUTA KUSHIBA TU. MFANO MDOGO NI HUU WA MADIWANI ARUSHA WAMEGUNDUA WENZAO WABUNGE WA CHAMA CHAO WANAKULA WANASHIBA HALAFU WANAKAZANA KUWAZUIA WENZAO WASIWE VIONGOZI NA HIVYO POSHO ZINAWAPITA MBALI WAMEAMUA KUGOMA MAAZIMIO YA CHAMA CHAO KWA KUWA WAMEONA HII KUMBE IN DANGANYA TOTO TU

    ReplyDelete
  6. Nape, usijisahau kama wenzako yatakutokea puani kwani wewe bado ni mtoto. Ongea kama mtu mwenye hekima anachana na tabia za kishule. Ukiona yanaasemwa kuwa na tahadhari kwani maneno huchafua kuliko vitendo, achana na siasa za kiafrika na kuwa siasa za kiustaarabu kama nchi inayokomaa kidemokrasia. Kumbuka watu waliopoteza maisha huko Zanzibar wakati wa jutawala wa CCM, damu yao itakurudia kabla kukomma katika siasa. Nenda polepole, vinginevyo ukawa tambiko la waliomaga damu za watu. Watu siyo wanyama wana roho kama wewe. Sikia hilo na umwombe Mungu akukinge na kiburi, ulionekana na mwelekeo, naomba ujitafakari tena katika wajibu uliokabidhiwa na umma bila kuangalia itikadi ya chama chochote kile.

    ReplyDelete
  7. Wote wanatafuta kula tu hakuna lolote la maana. Nchi ina miaka 50 tangu Uhuru imeshindwa hata kuwa na umeme wa uhakika.Raslimi zote ziko tz mungu kaijaalia. Kila kukicha uchumi ndio kwanza unadidimia. Pumbavu wakubwa tokeni waachieni wengine nao watafute riziki zao.

    ReplyDelete
  8. NADHANI MHE.PINDA KAMA UTAKUMBUKA WAJIBU WAKO UKIWA NI KIONGOZI WA SEREKALI NA NI KUHAKIKSHA NA KUPENDA AMANI INATAWALA KATIKA NCHI YAKO UNAYOIONGOZA NI UKWELI USIOPINGIKA KWAMBA KAULI ZA NAPE SI ZA KUCHILIWA KWANI KAMA HAZITAKEMEWA NA KUENDELEA ZITAKUWA NA ATHARI BAADAE,USINYAMAZE AU KUZIBEZA TU KWA SABABU ZIMETOLEWA NA KIONGOZI WA CHAMA CHAKO JE INGEKUWA NI KIONGOZI WA UPINZANI UNGEKAA KIMYA PIA? PIA UKIANGALIA KWA MAKINI YEYE HUYO NAPE INAMUHUSU NINI NA MAMBO YA SERIKALI YA ZANZIBAR KAMA ANAJUA KUCHONGA MDOMO SI ACHONGE HUKO KWAO NA KWA HAO WALIOMPA HUO ULAJI NA KUJIFANYA NI MSEMAJI SANA USHAURI WANGU NI KWAMBA MAMBO YA ZANZIBAR AWAACHIE WAZANZIBAR WENYEWE KUAMUA SIO YEYE ACHONGE MDOMO WAKE.WAZANZIBARI WENYEWE WAMERIDHIKA SASA YEYE ANATAKA NINI,ANATAKA KUNIAMBIA ATAKAPOVULIWA HAYO MADARAKA ALIYONAYO HATOLlMIKA?

    ReplyDelete
  9. MIMI NADHANI NAPE BADO UNA UKILI ZA KITOTO NA KWA KWELI HUFAI HATA KUWA KIONGOZI WA KATA ACHILIA MBALI WILAYA,HAO WALIOKUPA HAYO BADARAKA NADHANI WALIKOSEA SANA KWA UFUPI HUFAI NA WALA AKILI ZAKO HZIJATULIA NI VYEMA UKARUDI SHULE KULIKO KUTOA KAULI ZA KIJINGA KWENYE MIKUTANO YAKO NA HAO WAPUMBAVU WANAO ACHA SHUGHULI ZA KUJITAFUTIA RIZIKI NA KUKAA WAKAKUSILIKILIZA HIZO POROJO ZAKO UNAZOZITOA KWA KWELI HUFAI HATA KUWA KIONGOZI WA KISIASA KWANI SIASA ZAKO ZINAONEKANA NI ZA MASKANI NA NI IMANI YANGU UTAKAPO ENGULIWA HAPO SIJUI UTAFANYA NINI? INAONEKANA HATA AKILI ZAKO HAZIJATULIA VIZURI NA USHAURI WANGU KWAKO NI KWAMBA FIKIRI UZURI KABLA YA KUROPOKWA NA MIJINENO YAKO ISIYO NA KICHWA WALA MIGUU UNACHATAKIWA HAPO UIKEMEE SERIKALI ISINYANYASE WANANCHI WAKE MIAKA HAMSINI YA UHURU LAKINI HATA UMEME HAKUNA NA NYINYI MNATEMBELEA MAGARI MAZURI NA KUFUGA VIMADA KWA WINGI MITAANI BASI KWA UFUPI CHUNGA DOMO LAKO HILO KABLA YA KULIFUNUWA NA KUHANIKIZA HARUFU MBAYA

    ReplyDelete
  10. Namkumbusha Nape kwa msemo maarufu wa zamani "Mtaka nyingi nasaba, humfika mwingi msiba na mchamba kwingi, huondoka na mavi". Nini walichokipata kina Hiza Tambwe na wenzake pamoja na yule mama wa Pemba na kaka yake?

    ReplyDelete
  11. Tumhadhirishe huyu Nape, kwakuwa anajaribu kuja juu kama moto wa vifuu. Huyu ndie atayeiangamiza Tanu chama ambacho kilicholeta uhuru na nchi ikaendelea na amani mpaka leo hii. Huyu kijana anachokitaka ni ukubwa, lakini naona hafai kwasababu ana chuki na aangaliwe kwa macho mawili. Vipi huyu anathubutu kufunguwa mdomo wake na kumkejeli Maalim Seif ambaye amechukwa sehemu kubwa kuleta amani huko Zanzibar. Yeye huyu alikuwa anataka chuki na mauwaji yaendelee na kutokana na hayo vipi Mungu akubaliane naye ili awe kiongozi? Hivi sasa tulivo CCM ipo katika wakati mgumu sana na huyu jamaa badala ya kutamka maneno ya amani na upendo amekuwa akiwakejeli viongozi waliochaguliwa na wananchi wao huko visiwani. Huyu sasa angojee fimbo ya Mungu tu.

    ReplyDelete
  12. Siasa za serikali ya umoja ni kukubaliana ufisadi kuufanya pamoja na kuwarubuni wananchi ya kuwa sasa wao kwa vile wameafikiana kukka meza kuu na kumtafuna kuku kwa mrija basi nao waridhike.......................ni usaliti usio na kifani......................sijui Nape alisema nini lakini huo mwafaka una manufaa kwa viongozi lakini siyo wanancni.......nini maana ya siasa za ushindani kama mwisho wake ni kuwa hakuna ushindani?????????????????

    ReplyDelete
  13. Nape ni nepi,ndio matatizo ya watoto wa kufikia,baba yake wa kufikia alikuwa na busara mno,angemzaa yeye, Nape angerithi japo robo ya busara zake,lakini ashukuru kuruhusiwa kutumia ubini wa Mnahuye kwani ndio uliomfikisha hapo alipo.

    ReplyDelete
  14. kutoka mtoto wa mkulima mpaka mtoto wa fisadi aliyepinda. (mizengwe pinda)kutoka mtoto wa mkulima mpaka mtoto wa fisadi aliyepinda. (mizengwe pinda)

    ReplyDelete
  15. huko ccm mambo ni hasi tu.siasa za majungu,hawahui kusonga mbele,wamepewa madaraka,wanaogogpa kazi,wanakimbizana na chadema tu.wale wapinzani wao wako chanya,safu yao wasomi watupu,wanaona mbali,wanagundua mengi.kama sio wao kuwa chanya haya ya nishat mngefunika tu kama kawaida yenu.zito kawatoa kamas,na bado,huyo nape atazidi kuwadumaza,na kuwa hasi hadi kiama chenu.zindukeni,achen siasa za maji taka.mnapingana wenyewe kwa wenyewe mliona wapi.gamba haliwezi kutoka kwa nyoka hai labda huyo nyoka afe,ndo gamba litatoka vizuri.kumekucha.

    ReplyDelete
  16. ushamba wa madaraka tu....walikuwepo kama yeye...

    ReplyDelete
  17. nadhani Mh. Pinda ana ukweli katika aliyoeleza. Hakuna sababu ya kumcharukia. Kama kiongozi anapaswa kufanya uchunguzi ili ajiridhishe na ajibu kama inavystahili. Subira yavuta heri. Siasa za kupayuka sio siasa. Chadema wanafanya vyema , wanachunguza, wanatafakari na kisha wanasema, Huo ndio umakini unaotakiwa.

    ReplyDelete