20 July 2011

Essien azua mzozo kwa Ghana, Chelsea

LONDON, Uingereza

KUUMIA tena kwa kiungo Michael Essien, kumesababisha klabu yake na nchi yake kuzozana.kwa mujibu wa Daily Mirror, kiungo huyo atakaa nje ya uwanja kwa miezi
sita baada ya kuumia katika goti la mguu wa kulia.

Ghana imekuwa ikiogopeshwa na Essien, ambaye hakucheza katika mechi 16 za timu ya taifa anaweza kukosa tena kucheza kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa mwakani.

Endapo Essien atakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kama inavyodai Chelsea, atakaa nje hadi katikati ya Januari mwakani siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Ghana kwa upande mwingine inapanga kutuma timu ya madaktari wake kufuatilia hali ya  Essien.

Msemaji wa Ghana aliiambia Sportsmail: "Kuna dalili kuwa atakuwa nje kwa miezi sita. Pia tunajua kuwa Michael, yuko imara kiakili na tuna matumaini atapata nafuu kwa haraka.

"Tumekuwa na mahusiano mazuri na Chelsea na tutaendelea kuzungumza nao kuhusu kupona kwake.

"Kama tunaona inafaa kumtuma daktari mmoja kwenda London, hatutasita kufanya hivyo."

Ghana imekuwa ikitofautiana na Chelsea kuhusu kumkataza mchezaji huyo kuchezea timu ya taifa kwa madai ni majeruhi katika kipindi cha nyuma, sasa inaonekana inaweza kuwa hivyo.

Mara ya mwisho Essien, alichezea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2009-10 na kukosa mechi za mwisho za Chelsea.

No comments:

Post a Comment