21 July 2011

Diwani aamuru mgambo wapigwe mawe

Na Flora Amon

DIWANI wa Kata ya Sinza kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Renatus Pamba ameamuru wananchi kuwapiga mawe mgambo feki
wanapoenda kuwakamata wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza na Majira diwani huyo alisema kuwa kumekuwa na kuchafuliana majina baada ya watu wasiojulikana kuweka mgambo ambao hawatambuliki kisheria kuwakamata wananchi, hivyo kuleta mtafaruku.

"Ni kweli mwandishi nimawaamuru wananchi wa Sinza kuwapiga mawe mgammbo feki wanaokwenda kuwakamata, na kuwalipisha faini kinyume cha sheria," alisema.

Aliongeza kuwa mgambo ambao wamewekwa kisheria wanatambulika mpaka manispaa, lakini cha ajabu kuna mtu asiyefahamika na yeye katafuta mgambo wake na mbao wanafanya hivyo kinyume cha sheria kutokana na chuki za kiasa na kutaka kumchafulia jina.

Aidha alisemakuwa ameshatoa taarifa katika Kituo cha Polisi kuhusu mgambo hao na wanaendelea kuwatafuta kufahamu nani amewapa mamlaka hayo bila yeye kuwatambua.

Mmoja wa Polisi Wasaidizi Kata ya Sinza ambaye hakupenda jina lake liiandikwe gazetini alisema kuwa ameshangaa kitendo cha diwani huyo kuruhusu wananchi kuwapiga mawe pale wanapoenda kuwakamata wakitumiwa kwa uchafuzi wa mazingira.

Alisema kuwa wameajiriwa na Manispaa ya Kinondoni na kugawanywa katika kata mbalimbali, kwa ajili ya kusimamia sheria ambapo mtu akikiuka anachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kupelekwa ofisini na akionekana ana kosa hutozwa faini.

"Sasa nashangaa kitendo cha diwani katika mkutano wa hadhara na wakazi wa Sinza D Jumamosi kuamuru kupingwa mawe askari mgambo wakati wapo katika kuteleza majukumu yao," alisema.

1 comment:

  1. Pale nchi inaposhindikana kutawalika ndio mambo kama haya yanjitokeza! Mi nasema hewala bwana changu ni changu na chako ni chako!

    ReplyDelete