14 July 2011

20 Percent kutumbuiza Usiku wa Kopo

Na Addolph Bruno

WASANII wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature, Daz Baba na 20 Percent wanatarajia kutoa burudani katika 'Usiku wa Kopo' unaotarajia kufanyika Julai 22, mwaka huu
katika viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.

Usiku huo maalumu umeandaliwa na Kampuni ya Entertainment Masters Limited ya Dar es Salaam, ambao ni maalumu kutoa shukrani kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa kukichangia kituo cha televisheni cha DTV kuwa bora.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Penniel Mungilwa alisema lengo la usiku huo ni kuwapa burudani wakazi wa Temeke na vitongoji vyake.

Aliwataja wasanii wengine watakaotoa burudani ni Mr Blue, Kundi la Gangwe Mob, Belle 9 pamoja na John Makini.

Alisema usiku huo maalumu utatawaliwa na nderemo na burudani mbalimbali ya muziki wa kizazi kipya pamoja na zawadi mbalimbali.

Mratibu huyo alisema katika usiku huo, wanafunzi wa vyuo mbalimbali watapata fursa ya kubadilishana mawazo, ambapo pia Ma-dj kutoka Klabu Maisha watafanya vitu vyao.

No comments:

Post a Comment