08 April 2011

Mbozi wapata kikombe cha kunyunyiza

Na Charles Mwakipesile, Mbozi

KIONGOZI wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji, Bw. Joshua Mwantyala wa Morogoro, juzi alianzisha huduma ya kugawa matone ya maji ya anayodai
yananya magonjwa mbalimbali ukiwemo Ukimwi, huku akiitaja huduma yake kama 'majibu ya maajabu ya Loliondo'.

Akizungumza wakati wa kutoa huduma hiyo, Mjini Vwawa Bw. Mwantyala alisema kuwa badala ya viongozi wa dini kuelekeza makombora kwa Mchungaji Ambilikile Masapila 'Babu' wa Loliondo, wanatakiwa kukaa kwenye maombi ili Mungu awape ufunuo mpya kama alivyompa yeye.

Alisema kuwa yeye alipewa ufunuo huo mwaka 2009 akiwa mjini Morogoro, aliwaomba watengenezaji wa maji ili aweze kubandika nembo ya Yesu katika maji hayo na walipokubali, alianza kazi ya kugawa matone, na kila aliyekunywa alipona magonjwa yake yaliyokuwa yanamsumbua.

“Nnajua Mungu amemleta Mchungaji Ambilikile Masapila wa Loliondo kwa wakati wake, lengo lake ni kutaka watu wake wapone na kisha aweze kuleta uponyaji mwingine mkubwa zaidi ya huu wa Loliondo, huu ndio mpango wa Mungu, na hata hapa Mbozi watu watapona zaidi,” alisema, kisha akaanza kuwamiminia maji kinywani watu waliofika kupokea huduma hiyo.

Bw. Mwantyala anayejitaja kama nabii, alisema kuwa hakuna haja ya Watanzania kuendelea kuhangaika kwa sasa kwa kwenda kwa waganga badala yake wamwamini Mungu na kupokea matone hayo ya maji ambayo alisema atayagawa nchi nzima  kwa kupita kwenye wilaya zote.

5 comments:

  1. mbona hamuoti hatma ya Dowans na katiba mpya?????

    ReplyDelete
  2. KUNA HAJA YA KUWA MAKINI NA HAWA WANAOJITOKEZA KAMA MANABII. mANABII WA UWONGO WATAJITOKEZA NA KUVURUGA HUDUMA YA KWELI INAYOTOLEWA HUKO LOLIONDO. TUWE MAKINI KWA SABABU KAMA HUDUMA HIZO NI ZA KWELI, UKWELI HUO UTAJITOKEZA TU. KWANZA TUBAKI MZEE WA KIKOMBE HUKO LOLIONDO. TUWE MAKINI ILI TUSICHAnganyikiwe na kuacha huduma ya kweli ambayo mungu amemwonesha Mchungaji wa Loliondo.

    ReplyDelete
  3. Mungu alisema siku ya mwisho kutakuwa na manabii wauongo ambao watalitaja jina lake, na watu kuwaamini.

    Hivyo basi watanzania msimuamini kila mtu atakayejitokeza kuwa anaponya magonjwa sugu mara ameoteshwa na Mungu hapa, kwanini wasijitokeza mapema kabla ya Babu.

    Wa ukweli ni Babu wa Loliondo wangine hawa ni wababaishaji mbona kama ni hivyo watanzania tuna elekea kubayaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  4. Ana haki ya kufanya au kutoa huduma kama ananvyo amini yeye lakini asitulazimishe kuamini kwamba tiba yake ni kweli tunachojiuliza ni kwanini hakutoa huduma hiyo wakati wowote isipokuwa sasa? au anamuiga babu? lakin tukumbuke kuwa ktk imani ya kawaida si kawaida Mungu kujidhihirisha kwa watu zaidi ya mmoja. sasa kazi kwetu.

    ReplyDelete
  5. Manabii wa uongo hata kwenye uislam wametajwa kama Masihdajali. Hii ni pamoja na babu wa loliondo. Kufa mwanadamu ni wajibu. na hivyo anayezuia kifo ni muongo.

    ReplyDelete