18 April 2011

Jumuiya CCM zatakiwa pia 'kujivua magamba'

Na Gladness Mboma

MWENYEKITI wa Taifa CCM, Jakaya Kikwete pamoja na sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, Bw. Wilson Mukama wameombwa wayafikishe mageuzi katika ngazi zote
za chama na jumuiya zake ili kuwaondoa viongozi wote wazembe, wasio waadilifu na wafuasi wa mafisadi.

Mbali na ombi hilo pia wameombwa katika chaguzi zitakazokuja kiandae utaratibu utakaowazuia mafisadi na washirika wao wote kugombea na kupata nyadhifa ndani ya chama, na kuwa makini nao kwa kuwa hivi sasa wana hasira na chama.

Hayo yalisemwa jana na Shirikisho la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam,  wakati likimpongeza Rais Kikwete kwa 'ujasiri na hatua madhubuti' alizochukua katika kufanya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya CCM.

"Kama chama kitakubaliana na ombi letu la kuandaa utaratibu utakaozuia mafisadi na washirika wao wote kugombea na kupata nyadhifa ndani ya chama, hilo litarudisha imani kwa wafuasi na wanachama wa CCM, hali itakayokifanya chama kibaki kuwa kimbilio la wanyonge, wakulima na wafanyakazi," alisema Katibu wa Shirikisho hilo, Bw. Abubakar Asenga.

Alisema kuwa wanaunga mkono hatua zilizoanzishwa na chama za kupambana wazi na vitendo vya kifisadi na kwamba wale wote ambao wanatuhumiwa kwa kashfa nzito za ufisadi mkubwa na ubadhirifu wa mali za umma waachie nyadhifa zote ndani ya chama katika muda wa siku 90 walizopewa.

Bw. Asenga alisema watuhumiwa hao wasipofanya hivyo, wao (vijana) wataunga mkono hatua za chama kuwang'oa, na kusisitiza kwamba CCM siyo kichaka cha kuhifadhi watu wasio waadilifu wala mafisadi, na akawashauri waachane na siasa wakafanye biashara.

Katibu huyo alisema kuwa wanaunga mkono mageuzi makubwa yaliyofanywa kiuongozi, pili dhamira ya kufanya mchakato wa marekebisho ya kimfumo ndani ya chama.

"Shirikisho linatoa pongezi za dhati kwa sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, Bw. Mukama, uteuzi wao ni faraja kubwa kwa chama, hasa kwa kuwa umezingatia hali halisi ya siasa za sasa na uwakilishi wa vijana ambao ndio wadau wakubwa," alisema.

Bw. Asenga aliwapongeza pia wote waliochukua hatua za kujiuzulu nafasi zao, ili kupisha mageuzi makubwa ndani ya chama licha ya kwamba ni maamuzi machungu, lakini yanayofaa kupongezwa na kuigwa.

Shirikisho hilo limewataka vijana nchini kupeleka maoni na mawazo yao katika matawi na kuacha kutumia utaratibu wa kuropoka hovyo.

Alisema kuwa mafisadi watakuwa wanawatumia vijana ili UVCCM ionekane haijatulia na kuwataka kukaa chonjo na kundi hilo ambalo kwa sasa lina hasira na chama.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Godluck Mangomango ambaye alidai alikuwa mwanachama wa CHADEMA amejiunga na shirikisho hilo kwa madai ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Bw. Mangomango alisema kuwa baadhi ya vijana waliokuwa wamejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA, sasa wameamua kurejea CCM baada ya kuwepo kwa mabadiliko.

5 comments:

  1. Ina maana huyo Mangomango alikimbia CCM kwa ajili ya Makamba au sera mbovu,huyu ni opportuist mbaya sana na hatafika mbali kama anategemea future yake kwenye politics,bora afikilie biashara nyingine,najua watajitokeza wakina Mangomango wengi msimu huu wanaojaribu bahati zao kwani ni kweli politics is a game of chance.

    ReplyDelete
  2. NAWASHANGAA WANAOMPONGEZA RAIS KIKWETE NA CCM KWA "UJASIRI"! ANGEKUWA JASIRI ASINGEPEMBELEZANA NA MAFISADI TANGU 2005 MPAKA 2011 HUKU AKIBAKISHA MIAKA MITATU ATOKE. ASINGEWAPA WEZI MUDA WA SIKU 90 KIJIONDIA CCM. KWA MANENEO MENGINE BADO WEZI WAKE ANAO HATA SASA. HUO NDIO UJASIRI???KUMBUKA HATA WEZI WA EPA WALIPEWA MUDA WA KURUDISHA PESA ZA BOT, MPAKA LEO WAKO HURU. HUO NDIO UJASIRI? NA HAO WEZI WA KUKU MBONA WANAFUNGWA TUU? HUYU SPIKA WA UDSM NI MSOMI GANI ASIYEKUWA NA UWEZO WA KU ANALYSE MAMBO? CCM DANGANYA TOTO TU NI WEZI TU . NITAMWITA KIKWETE JASIRI SIKU ATAWABURUZA MAHAKAMANI LOWASSA, CHENGE, KARAMAGI, SOMAIA, KOMBA,ROSTAM,MAKAMBA,IDRISSA RASHID,MEGHJI NK. BADALA YA MEGHJI KUPUMZISHWA KWA KUSIGN PESA ZA EPA ANAPEWA UJUMBE WA CC YA CCM? MNACHEKESHA CCM. KUMWONDOA MAKAMBA NA KUMZAWADIA MTOTO WA MAKAMBA CHEO! CCM WANATAKIWA KUONDOLEWA BILA HURUMA. LAZIMA TUKUE WATANZANIA!!!

    ReplyDelete
  3. Naamini Tanzania vijana wetu wanaoitwa wa vyuo vikuu na wa umri huo wachache wao BADO wana matatizo MAKUBWA vichwani mwao kama huyu spika. Pia niliona barua iliyoandikwa na BASHE kwa seketariati mpya ya CCM nikashangaa na kuona huruma. Niliwaza kama huyu ndiye kiongozi wa vijana wa ccm kwa tazania nzima, basi hatuna haja ya kujivunia na vijana wa aina hii. Uandishi mbovu, kiingereza hovyo, kiswahili hovyo, nukta, koma nk hazina mpango achilia mbali mantiki...halafu vijana wanampigia kura kwamba yeye ndiye kiongozi wao. kuna tatizo kubwa kuliko tunavyodhani. Nawasihi vijana wenye uwezo, uzalendo na thubuthu waingie kwenye siasa acha hawa wanaotetea na kuzolewa na mafisadi wa CCM. CHADEMA OYEE!

    ReplyDelete
  4. KILA KITU KINA MWANZO WAKE NA MWISHO WAKE. SIKU ZOTE MWANZO NI MGUMU ILA TUMEUONA.
    TATIZO LANGU KUBWA, NI KUONA JUHUDI HIZI HAZIWI NGUVU YA SODA. WATANZANIA WOTE TUMESHUHUDIA MALUMBANO NDANI YA UV-CCM NA KAULI YA MWENYEKETI WA UWT-CCM AKIWATETEA KWA NGUVU ZOTE MAFISADI. BILA SHAKA ANAPENDA KUONA HAKI IKITENDEKA KWA MAFISADI AMBAO NI WAFADHILI WAKE AU MARAFIKI WA KUFA NA VIJISENTI. HUYU NA WASAFISHAJI WENGINE NAWAPA MFANO HUU... UKIMUONA SIMBA AMETAPAKAA DAMU MWILILINI NA BAADAE UKASIKIA KUWA USIKU ULIOTANGULIA KUNA WATU KATIKA MJI WA JIRANI WAMELIWA NA SIMBA, JE UTACHUKUA HATUA GANI?? KWA YEYE NADHANI ANATAKA TUTAFUTE DNA KUTOKA KWA SIMBA NA MASALIA YA MAREHEMU WETU, NDIO TUSEME SIMBA KALA WATU..MWENYE AKILI NA ATAMBUE HILO. SOMA KITABU CHA TUJISAHIHISHE CHA MWL JK NYERERE.

    ReplyDelete
  5. mangomango,,,,another hiza tambwe!! ataangukia pua tuu

    ReplyDelete