11 April 2011

Hughes aitabiria ubingwa Man United

LONDON, Uingereza

MARK Hughes juzi alishuhudia timu yake ikifungwa dhidi ya Manchester United na kisha akatabiri kuwa miamba hiyo, inaweza kutwaa makombe matatu msimu
huu.

Mabao mawili ya Dimitar Berbatov na Antonio Valencia, yaliifanya United  kuzidi kuendelea kuwa kinara wa Ligi Kuu wakiongoza kwa tofauti ya pointi 10.

Na kocha wa Fulham, Hughes alisema kuwa klabu yake ya zamani inaweza kufikia rekodi yake ya mwaka 1999, kwa kutwaa makombe ya Ligi ya Mabingwa na FA.

Hughes alisema: "Wanaweza kutwaa kila kitu.

Alisema wamekuwa wakishinda mechi, kitu ambacho ni muhimu katika kipindi hiki cha msimu, wanajua ni kitu gani wanataka.

Kocha huyo alisema ni ngumu sana kufanya kitu kama hicho, lakini timu ya Sir Alex imekuwa ikifanya hivyo.

"Lakini nina amini mimi ni kitu ambacho watajaribu na kufanikiwa. Kila la kheri kwao."

Ila wakati Hughes akiipongeza United, kocha wa Old Trafford, Alex Ferguson aliwalaumu wachezaji wake kwa kutocheza vizuri pamoja na kupata mabao mawili katika muda wa dakika 32.

Alisema: "Ilikuwa ni matokeo lakini siwezi kusema ilikuwa ni kazi iliyofanywa vizuri.

"Kipaindi cha kwanza tulicheza soka nzuri sana na tungeweza kufunga magoli mengine zaidi."lakini tulipoteza umiliki wa mpira katika kipindi cha pili na tungeweza kupata matatizo kwa hilo."

Mcheazaji wa Chelsea anayecheza kwa mkopo Fulham, Gael Kakuta alianza kucheza kwa mara kwa kwanza akiwa chini ya Hughes.

Alimjaribu kipa mbamba mbili wa United, Tomasz Kuszczak ambaye alicheza badala ya Edwin van de Sar.Nani alicheza vizuri na kusaidia kupatikana kwa mabao yote mawili ya United.

United ingeweza kupata panalti, lakini mwamuzi Michael Jones hakutoa baada ya Nemanja Vidic kumnawisha mpira Dickson Etuhu.

Moussa Dembele wa Fulham naye alimjaribu kipa, Kuszczak  mwishoni mwa mchezo ambaye alipangua shuti lake na kisha Bobby Zamora naye alipaisha mpira alipokuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.

No comments:

Post a Comment