05 April 2011

Cameroon watua kuikabili Vijana Stars

Na Addolph Bruno

TIMU ya soka ya taifa ya vijana ya Cameroon wenye umri chini ya miaka 23, imewasili nchini jana kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kushiriki
fainali za Olimpiki dhidi ya Vijana Stars, utakaochezwa Jumamosi Jijini Dar es Salaam.

Awali Vijana Stars ilicheza na Cameroon Machi 27 mwaka huu Jijini Younde nchini humo na ilifungwa mabao 2-1.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Boniface Wambura, alisema hadi jana mchana  haikufahamika timu hiyo inawasili na wachezaji wangapi kutokana na wao kushindwa kutoa taarifa mapema.

"Tumepokea taarifa yao asubuhi ya leo (jana), kwamba wanakuja saa tano na nusu na kutokana na ucheleweshwaji wa taarifa hatukuweza kujua timu itakuwa na watu wangapi na sisi tuweze kuwatumia viza lakini hatukuweza," alisema Wambura.

Alisema timu hiyo itafikia katika hoteli ya Durban na kuanza mazoezi siku yoyote kuanzia leo, kabla ya mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja ambao watawaandalia.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu ya Vijana Stars, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema maandalizi kuhusu mchezo huo yanaendelea vizuri ambapo kesho atazungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo huo.

1 comment:

  1. TFF na TBC mechi hii ni tukio la kitaifa. Mkumbuke Tanzania si Dar es Salaam tu, ni Pemba, Unguja, Mwanza, Makete,Bumbiti,Kibondo...tunataka tuone mechi kwa vyovyote vile...onesheni mechi hii katika TV. Msitangulize pesa mbele.Morale ya kupenda timu za taifa imeshuka sana...ili kuirejesha ni lazima muoneshe mechi.Ni aibu TV ya Taifa kutokuonesha mechi kama hizi...KBC,UBC zote hazikosi kuonesha mechi za timu ya Taifa.Msipoonesha mechi za vilabu hatutalalamika sana...ila Timu ya Taifa ni habari nyingine...

    ReplyDelete