07 March 2011

Benitez, Dalglish wachochea Ferguson kufungiwa

LONDON,Uingereza

MAKOCHA wawili  Kenny Dalglish na Rafa Benitez  wameungana katika kumshutumu kocha mwenzao Sir Alex Ferguson kwa kuwa na tabia ya kupenda
kuwashambulia waamuzi kwa maneno ya kuwadhalilisha marefa wakiungana na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter.

Dalglish alitoa shutuma hizo kabla ya pambano kati ya timu yake dhidi ya United jana kwenye uwanja wa Anfield.

Kocha huyo pamoja na kocha wa zamani wa Liverpool, Benitez wametaka mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya Ferguson kutoka na hatuzi yake ya kuwafokea na kuwadhalilisha marefa.

Ferguson mara kwa mara amekua akiwashambulia waamuzi, kinyume na kampeni ya FA ambayo imekuwa ikiwataka makocha kuwaunga mkono waamuzi.

Na Dalglish na Benitez wameitaka FA kuchukua hatu ya kutoa adhabu kwa watu wanaopingana na kampeni yao.

Dalglish  alisema: " Nimekuja kujua kuhusu kampeni baada ya kurejea katika ukocha. Ni kitu ambacho tunatakiwa kuheshimu.Marefa hufanya makosa, ni ngumu kwao kutofanya makosa. Lakini sisi pia tunafanya makosa.

Kocha wa zamani wa Liverpool  Benitez alisema: "Wao wanafanya mambo sahihi ambayo huwa na faida. Na kwa watu ambao hawafanyi hivi, mtu anatakiwa kusema, "inatosha inatosha .'

Ferguson, ambaye kwa sasa yupo hati hati kufungiwa mechi tatu na FA, alimshambulia refa Martin Atkinson aliyechezesha mechi katika United dhidi ya Chelesea ambayo timu yake ililala mabao 2-1.

Kocha huyo ametakiwa na Rais wa FIFA Blatter aonyeshe kujiheshimu mwenyewe.

Blatter, akiwa Newport katika mkutano wa FIFA akijubu swali kuhusu tabia ya Ferguson dhidi ya marefa alisema: 'Heshima inaanzia kujiheshimu mwenyewe. Hiki ni kitu ambacho tunakitaka kufanyika kila sehemu, kuanzia timu za vijana kuja juu."

Ferguson anadaiwa kuwaambia rafiki zake kuwa anakataa kuzungumza na vyombo vya habari kutokana na kutomtendea haki, ikiwemo hata televisheni ya timu yake, MUTV, ambayo mahojiano aliyofanya nayo yalisababisha kufunguliwa mashitaka na FA.

No comments:

Post a Comment