07 February 2011

Serikali kuandaa kongamano la michezo

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeandaa kongamano la michezo, litakalowakutanisha wadau mbalimbali wa michezo nchini.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu alisema kongamano hilo litangazwa hivi karibuni lengo likiwa ni kuviweka vyama vya michezo karibu.

"Kongamano hili tulipanga tulifanye tangu mwaka juzi, lakini hata mwaka jana ilishindikana ila kwa mwaka huu kama serikali tumejipanga kuhakikisha tunalifanya, ili kuwakutanisha wadau pamoja kupeana mawazo ya nini tufanye ili michezo yetu ipige hatua," alisema Kipingu.

Alisema hiyo itakuwa ni rahisi kwa kila wadau kutoa mawazo yao, ikiwa ni pamoja na kujua nini kifanyike ili wadau hao waweze kuwekeza udhamini wao kwenye michezo ambayo mingi imekuwa ikikosa udhamini.

Kipingu alisema bado mchakato wa matayarisho ya kongamano hilo yanaendelea na kwamba tarehe na wapi kongongamano hilo litafanyika, watatangaza baadaye ili wadau wote waweze kujipanga.

No comments:

Post a Comment