Na Agnes Mwaijega
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watu 43 kwa tuhuma za unyang'anyi wa kutumia nguvu. Watuhumiwa hao walikamatwa
katika operesheni kali ya kuwasaka wahalifu iliyofanywa na jeshi hilo katika kipindi cha wiki mbili katika maeneo tofauti ya jiji.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa kuanzia Februari 14 hadi jana katika mikoa ya kipolisi ya Ilala, Temeke na Kinondoni.
"Operesheni hiyo ni endelevu na ni kwa ajili ya kuweka jiji katika hali ya utulivu na amani," alisema.
Bw. Kova pia alisema jeshi hilo kupitia kitengo chake maalumu cha kudhibiti wizi wa magari kimefanikiwa kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za wizi wa magari matatu.
Magari hayo ambayo na Toyota Hiace yenye namba za usajili T 968 AKW mali ya Fred Mashinde, Toyota Land Cruiser Prado yenye namba za usajili UAM 244 ambayo iliibwa uganda na Toyota Costa yenye namba za usajili T 757 AUK mali ya Iddi Kamjingijingi.
No comments:
Post a Comment