04 February 2011

Pinda aonya wabunge kutokuwa waropokaji

Na Benjamin Masese

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amewataka wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za uendeshaji wa chombo
hicho na kuepuka kusema mambo wasiyokuwa na uhakika wala kuyafanyia utafiti.

Alisemwa hayo Dar es Salaam jana wakati akifunga semina ya siku 10 ya wabunge ambapo aliwataka kufanya kazi kwa umakini na kuepuka mitego ya makundi ya watu wenye nia mbaya na kwa maslahi binafsi.

Bw. Pinda alisema kuwa wabunge wote wanatakiwa kutumia muda wao mwingi kusoma kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa kuendesha Bunge hali ambayo itaondoa usumbufu kwa wengine kuwasomea vifungu elekezi juu ya jambo husika.

Aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha hali ya usalama wa nchi, umoja, amani, utulivu na mshikamano.

"Ifikie wakati wabunge tuepuka kutamka kitu tusichokijua vizuri au kukifanyia utafiti, hivyo kuna haja kubwa kwa mbunge yeyote kufanya kazi kwa maslahi ya chama, taifa, wananchi, jimbo pamoja na dhamira yake mwenye,"alisema.

Bw. Pinda alisema kuwa wabunge wanatakiwa kutumia fursa zao za uwakilishi kutembelea majimbo mengine ya mikoa mbalimbali ili kujifunza zaidi pamoja na kujua changamoto za jumla zinazowakabili Watanzania wote.

Akizungumzia hali ya wabunge waliyoionesha wakati wa semina hiyo, alisema kuwa mawazo ya wabunge na mada mbalimbali zilizowasilishwa, zimeonesha ukomavu mkubwa na ni dalili njema kwa Bunge lijalo.

Akijibu ombi lililotolewa na Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani kutaka serikali kuboresha maslahi ya wanansheria nchini ili kuongeza ufanisi wa kazi, alisema kuwa suala hilo litafanyiwa kazi haraka na kuahidi kulitolea tamko rasmi.

Hata hivyo Bw. Pinda aliwataka wabunge wote kushirikiana na kuondoa tofauti zao za kisiasa na kujipanga upya kuleta maendeleo kwa Watanzania na kuwasisitiza kuwa na uvumilivu.

Awali Spika wa Bunge Bi. Anna Makinda wakati wa kumkaribisha Bw. Pinda, alisema kuwa katika historia ya Bunge la Tanzania, semina hiyo imeweka rekodi ya mahudhuria na uchangiaji wa mawazo mazuri yenye dhamira ya kimaendeleo.

Bi. Makinda alisema kuwa mawazo yaliyotolewa na wabunge, yameonesha ukomavu wa wananchi kuwatambua wawakilishi wao wazuri wenye mwamko wa kuwakomboa kwa kuwaletea maendeleo.

6 comments:

  1. KAYANZA MIZENGO PETER PINDA wewe unaelewa kwa dhati ufisadi toka ndani halmashauri mpaka serikali kuu. unahitaji ushaidi gani kuzungumzia ufisadi huo uliokithiri? wakurugenzi na wakuu idara wanaogngoza kuwa na majumba ya kifahari zikiwemo guest houses and hotel. katika wilaya zetu watumishi wa serikali za mitaa ndiyo wanaongoza kumilki hayo majumba ya starehe hamjiulizi ni kwa mshahara gani mnaowapa hata kama wangetunza kwa miaka kumi na tano. tukipiga hesabu ya pesa ya serikali inayoibiwa kwenye serikali hiyo malipo ya Dowans ni mchezo na penaut!! sasa utakuta nyinyi mkitembelea wilaya mnawapongeza ee bwana umejitahidi? amejitahidi kwa kuuiba hela ya watanzania walalahoi? ili kurudisha ethics tufanye msako nchi nzima tuwaweke ndani na tufanye economic transformation . leo hii unawatisha wabunge waongee mambo waliyo na uhakika nayo hakuna mtu mzima aliyechaguliwa na watu akawa mtu wa kuunda maneno. hili la watumishi linahitaji ushaidi? hili la dowans ambalo wewe umefunga mdomo linahitaji ushaidi kuwawajibisha waliolipotosha taifa letu. mimi nimekushutukia sana mizenge tofauti na matarajio yangu sasa viongozi hawaorodheshi mali kwa taarifa yako magorofa yanayoibuka kama uyoga katika miji mbalimbali asilimia 30 -45% ni ya watumishi wa serikali! leo unatudanganya kuwa hutaki GX v8 kwanini usipige marufuku HASA UKIZINGATIA KUWA UNAYO MAMLAKA YA KUFANYA HIVYO?wewe si ndiyo waziri mkuu? itakumbukwa ulilia sana wakati waziri mkuu aliyepita lowasa alipokuwa anatamka kujiuzulu hivi unaweza kugusa lolote linalomhusu huyo bwana. WABUNGE SEMENI SAUTI ZENU ZISKIKE KWA WATANZANIA BILA KUJALI ITIKADI YA VYAMA VYENU NA UNGANENI KWENYE MAMNBO YA KITAIFA NA HATUTAKI KUSIKIA NANI ALIYEANZISHA HOJA TUNATAKA KUONA IMPACTS. huu ni mwaka mpya tutawa rank kwa hilo.

    ReplyDelete
  2. WIIIIIIIIIIIIZI MTUPU HATA DR SLAA MLISEMA MROPOKAJI NYIE, AU NAWE MTOTO WA MKULIMA USHAWAIGA WENZIO? MI NAWAWPENDA NA NAWAKUBALI WABUNGE WAROPOKAJI KM ALIVOKUA DR SLAA COZ WANAROPOKA VINAVYOROPOKEKA TU

    ReplyDelete
  3. Huyu naye wameshamchakachua

    ReplyDelete
  4. MIZENGO UMEGEUKA KUWA MR.MIZENGWE BAADA YA KU EXTEND DEBATE UNATAKA KU LIMIT DEBATE BAHATI MBAYA KAZI YA WAZIRI MKUU SIYO KUWAAMBIA WATU NINI WASEME NA NINI WASISEME UMEGEUKA KUWA MTETEZI WA MAFISADI HUKU UKIJIITA MTOTO WA MKULIMA ILI KUWAPOTEZA WAJINGA MALENGO WAKATI WEWE UONEKANI KUTETEA WALA KUPIGANIA PESA ZAO ZINAZOTAKA KULIWA NA DOWANS. KUANZIA SASA TUTAKUITA MTETEZI WA MAFISADI KWA SISI TUNAOANGALIA VITENDO VYAKO NA SIYO MANENO YAKO UNAYOONGEA JUKWAANI.WAKATI UNALILIA UTAFITI KTK MANENO YA WABUNGE WAKATI HUO HUO UDAI UTAFITI UFANYWE KWENYE MIKATABA ILI WATU WAONE NINI KILICHOMO, SIKUSIKIA UKIDAI UTAFITI UFANYWE KWENYE ISSUE YA DOWANS KABLA YA KULIPWA, SIJASIKIA UKIDAI UTAFITI DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA VIONGOZI WA SERIKALI WAKITANGULIZA MASHINGINGI MIKOANI HUKU WAO WAKIPANDA NDEGE NA WALA SIJASIKIA UKIDAI UTAFITI WA NANI ALINUNUA MASHANGINGI WAKATI ULISHATOA MAAGIZO YASINUNULIWE. UNADAI UTAFITI TU PALE UNAPOKUWA WAKUWALINDA WAKUBWA WENZAKO LAKINI INAPOKUWA KWENYE ISSUE AMBAYO UTAFITI UKIFANYIKA UNAMUUMBUA MKUBWA UNAFUKIA KILA KITU UKIDAI NI KUPOTEZA PESA.BAHATI MBAYA WATANZANIA WA SASA HATUANGALII MAJINA FEKI UNAYOJIPA TUNAKUANGALIA VITENDO VYAKO AMBAVYO NI KINYUME KABISA NA MANENO YAKO.

    ReplyDelete
  5. Hivi Mh. Pinda ni aibu gani hii mnatufanyia. Wewe ni mwanasheria kitaaluma, Kikwete ni Mchumi, Bilal ni .... n.k. bado tu mnahisi watanzania bado wamelala au ni wajinga sana baba?? Nyie wenyewe tu ndani ya mwezi mmoja mmetofautiana ktk suala la malipo ya DOWANS. na nahisi ulikuwa ukiiandaa paper yako/ mada hii ya haki na .... sasa leo wewe wasisitiza utafiti, are you serious with what you are propagating?? Ulifanya utafiti juu ya wajumbe wa CC, juu ya msimamo wa Rais, wabunge wa CCM......??? Maandiko matakatifu yanasema "Tutawatambua kwa matendo, sio maneno/ porojo ...." Acha siasa katika nafasi yako ya WM, Matendo ndiyo sifa ya nafasi hiyo. Unatakiwa ukisema jambo kila mtu anasikia na kutekeleza baba. Sasa Magufuli amekwishakufunika; whether anakurupuka au yuko katika mstari hilo ni suala jingine; lakini nakuhakishia endapo wananchi wangeulizwa nani awe Waziri Mkuu (WM) kwa sasa wengi wangemchagua/ wangempendekeza Magufuli. Kunja sura mwana!!! Hivi majuzi tu, Umekataa gari (Safiiiii sana) lakini wakataze na wengineo ili tujue umedhamiria. Sasa wewe wakataa, mawaziri na wakurugenzi wanaendelea kununua magari ya kifahari; hivi kuna akili hapo?? Mkurugenzi ana GX V8 wewe una pick up??? Unamhadaa nani ndugu yangu??? Kupitia ukaguzi wa CAG, nyumba ya gavana wa BOT imegharimu zaidi ya billion za kitanzania......kwa matengenezo tu??? Hivi tuna akili kweli watanzania wakati uchumi wetu ni mdogo, walio wengi wanataabika?? Hivi billion hizo ungetaka hata kujenga nyumba mpya, ungejenga ngapi baba?? Tena modern houses?? Aibuuuuuuuuuuuu!! Matokeo ya kidato cha nne ndiyo hayoooo umeyaona mheshimiwa WM. Sasa Mbunge akikwambia sera mbovu na za pupa katika utekelezaji wake, utahitaji afanye utafiti??? Imagine hili ni janga la kitaifa, lakini hujasema chochote; na nahisi hujamwita hata waziri wa elimu kukupa maelezo ili mpange mikakati ya kuondoa aibu hii. Hili ni bomu litakalopasuka si muda mrefu!! Wake up "Fake Peasant's son" Msituchefue akili na mioyo yetu bwana. Soma alama za nyakati na nenda na wakati. Crazy!!

    ReplyDelete
  6. kweli Pinda mtoto wa mkulima.

    ReplyDelete