04 February 2011

Majambazi yapora mil.15/- yatumia bunduki, mabomu

Na Faida Muyomba, Chato

KUNDI la watu zaidi ya 10 wenye silaha wamevamia duka la Wakala wa Kampuni ya simu ya Vodacom wilayani Chato, mkoani Kagera na kupora zaidi ya
sh. milioni 15 pamoja na vocha.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Bw. Vitus Mlolele, akizungumzia kwa njia ya simu na Majira, alisema tukio hilo lilitokea saa nane usiku wa kuamkia jana.

Alisema, kundi hilo, lilitumia baruti kuvunja duka hilo linalomikiwa na  mtu aliyetambuliwa kwa jina la Bw. Majura."Majambazi hayo yalitumia baruti kuvunja mlango wa duka hilo kisha kuingia na kufanikiwa kupora fedha taslimu sh. milioni 15 pamoja na vocha mbalimbali ambazo thamani yake bado haijajulikana,’’ alisema

Alisema, jeshi hilo bado linaendelea  na upelelezi wa kina kuwasaka watu hao na kwamba hakuna mtu aliyeuawa katika tukio hilo.

Habari zilizopatikana kutoka wilayani humo, zinasema kundi hilo la majambazi kabla ya kufanya uporaji huo, yalifyatua risasi kadhaa angani pamoja na kutupa mabomu ya mkono hali iliyozua hofu kwa wakazi wa mji huo.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema  watu hao walivunja duka hilo ambalo licha ya kuuza vocha za simu pia lilikuwa likitumika kutoa huduma ya M-Pesa kwa wateja wake.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Bi.Hadija Nyembo, alisema kuwa tukio hilo limewashtua na kwamba ameitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo.

"Ni tukio ambalo limetushtua mno na mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chato, nimehitisha kikao maalum ili tujadili kwa kina namna tutakavyopambana na hali hii ya uhalifu ambao unaonekana kutisha," alisema.

5 comments:

  1. polisi mko wap? hapo chato hamna kituo cha polisi ingaekuwa vyama vya upinzani ambao hata manati hawana mngetoka na K47 AU LMG lakini kwa wanaume wa shoka mnawasaliti wananchi kwa kulala chini ya mivungu ya vitanda vyenu. yuko wapi kamanda tossy uchaguzi umekwisha ameiweka dola kwa kutishia wananchi uko wapi sasa angalau urudishe imani kuwa unawalinda watanzania. tukio la senkenke na hilo la chato inaonekana kuna ushiriki wa polisi IGP CHECK OUT, usije ukawaunatafuta mchawi kikulacho ki nguoni mwako. muwajibishe kamanda wa mkoa.

    ReplyDelete
  2. We Bwana Anonymous hapo juu vipi? Unauliza swali la mfukoni? Katika nchi ambayo hata polisi wanashiriki katika ujambazi ni nini cha kushangaza kama majambazi yanatumia silaha za kivita kupora? Ipo haja ya kuuliza polisi walikuwa wapi?

    ReplyDelete
  3. hayo yameshakuwa ya kawaida Chato tunapafahamu lilikotokea tukio na kilipo kituo kikuu cha polisi na pua na mdomo yaani ukiwa hapo dukani unamwona aliyeko polisi sasa kama hawahusiki hapo ndio pagumu kwani hakuna hata risasi moja iliyorushwa kutoka polisi??? au ule usemi wa kituo cha polisi hakijawahi kufungwa ulikuwa wazama zile????

    ReplyDelete
  4. tunaamini hii ndio "intelligensia" ya Polisi Tanzania inafanya kazi.Hayo mabomu na risasi zikichunguzwa zitakuwa za taasisi ya uma yenye intelligensia. Kazi ikikosekana kwa vyama vya upinzani inahamia kwa raia. Intelligensia hizi zimeanza kuvunjwa huko Africa ya Waarabu. Na Inakuja huku. Hakuna intelligensia itakayoweza UMMA. UMMA UNAAMKA. UMMA UNAKUJA. Intelligensia kaeni chonjo.

    ReplyDelete
  5. acheni chuki na Polisi,kabla ujachangia lazima ifikirie binadamu tumetofautiana na wanyama katika kuchambua mambo.

    ReplyDelete