LONDON, Uingereza
KOCHA Alex Ferguson amefurahishwa na kiwango cha timu yake na kuweza kuwafunga mahasimu wao Manchester City mabao 2-1, Jumamosi na
kuzidi kujichimbia kileleni.
Ushindi huo umeiweka United katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kocha huyo amesifu wachezaji Wayne Rooney na winga wa kireno Luis Nani, baada ya wawili hao kufunga mabao yaliyoifanya United kupata ushindi, huku City ikipata bao lake pekee kupitia kwa David Silva.
Lakini, katika mabao ya juzi, Rooney alifunga bao la kusisimua la ufundi kwa kupiga tiktak, na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku ikiwa na pointi 57, na kuwapita wapinzani wao kwa pointi nane.
Fergie alitamba: " Bao lile lilikuwa lakusisimua, huwezi kuamiani.
"Bao la Nani lilikuwa ni la kusisimua, lakini kila mmoja alilisahau, hakuna hata mtu aliyelizungumzi, kila mtu anazungumzia bao la Rooney.
"Lilinikumbusha bao la Denis Law. Ilikuwa ni bao ambalo huweza kuamini."
Pia, Kocha wa City, Roberto Mancini, alilisifu bao lilifungwa na Rooney akieleza kuwa, lilikuwa zuri sana na kueleza kuwa, ndilo liliiua timu yake dhidi ya Manchester United.
Mshambuliaji huyo wa England alifunga bao hilo dakila ya 78, wakati matokeo yakiwa bao 1-1, na kuifanya United kupata bao la pili na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
City imeondoka na masikitiko kwa kutopata angalau pointi moja, wakiwa ugenini katika Uwanja wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment