11 January 2011

Mwandosya atoa angalizo CCM 2015

Na Moses Mabula, Tabora

VIONGOZI wa vyama vya siasa nchini, wametakiwa kuacha kusaka mchawi baada ya kushindwa katika baadhi yamaeneo na badala yake kuchapa kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.Kauli hiyo ilitolewa jana na mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), pia Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya wakati akipokea taarifa chama hicho mkoa wa Tabora, muda mfupi baada ya kuwasili katika ziara yake ya siku saba kukagua miradi ya maji.

"Sasa ni muda wa kazi tu, tena kwa kujipanga. Tusipofanya hivyo, mwaka 2015 hali kwetu itakuwa mbaya sana. Huu ni ukweli usiopingika kabisa. Tujitahidi kukamilisha ilani ya uchaguzi kwa yale yaliyopo," alisisitiza zaidi.

Profesa Mwandosya alisema litakuwa ni jambo ambalo halina tija kwa wanachama, viongozi wa vyama vya siasa, kuanza kusaka mchawi katika baadhi ya sehemu tulizoshindwa, muda ni mfupi sana katika kutekeleza ilani yetu ya uchaguzi, kwa kuwa wananchi tumewaahidi mengi ya kuwafanyia.

Alisema kuwa sasa hivi siyo muda wa malumbano bali viongozi waliochaguliwa kupitia vyama mbalimbali vya siasa watelekeze ilani ya serikali iliyopo madarakani na kuwaletea maendeleo wananchi. 

"Ndugu zangu muda ni mfupi sana katika kutimiza yale tuliyoahidi kwa wananchi, kwani sasa siyo miaka mitano tena bali ni miaka minne na miezi tisa tu tuliyobaki nayo, hivyo tunapaswa kufanya kazi ya ziada kumaliza kero zilizopo," alisema Mwandosya.

Waziri huyo aliongeza kuwa haitasaidia sana kuanza kuulizana wewe au nani alifanya tushindwe eneo fulani, haina tija na haiingii akilini katika kusaidia wananchi.

Alisema itafikia mahali muda umekwenda halafu tunaanza kuulizwa na wananchi kila kona kuwa tulisema hivi, lawama zitaturudia wenyewe kwa kushindwa kumaliza ahadi zetu.

Profesa Mwandosya aliongeza kuwa hakuna kitu kibaya kama wananchi wataamua kufanya maamuzi ambayo kwao ni majuto.

Alisema itashangaza zaidi kuwa baadhi ya viongozi na wanachama kuanza kutajana majina kuwa fulani alifanya hivi, kiongozi fulani alitusaliti, hiyo ni kujitafutia ama kujiletea mazingira magumu katika kusukuma
maendeleo.

3 comments:

  1. Acha hizo nawe unaanza kuwa kama shekhe yahya. Mbona hukukataa shangingi? ungejenga zahati ngapi? Maprofessa wa bongo sijui tulilogwa??? Nenda kwa kagame ujifunze maendeleo ni nini. Kila waziri anasema vyake. Hakuna serikali????

    ReplyDelete
  2. kafundishe chuo kikuu it is a shame maprofessors kuacha kufunndisha nakukimbilia siasa .Ni tz pekee utakuta watu kukimbilia taaluma zisizo zao.haiingii akilini rudi chuo kikuu hatimaye taifa hili litakuwa la wajinga kwani limepoteza maprofessors weng kwenye siasa huna maana angalia maji yalivyo yagharama tunazidiwa na watu wa zamani huko Engaruka! walikuwa na kilmo cha umwagiliaji we profesa mzima karne ya 21 hakuna tija ktk kilimo a u serious! ondoka! huna maana you will die with no title no legacy 2 hell with you are NONSENSE!

    ReplyDelete
  3. Mh.Mwandosya,atakaeiwa CCM ni Mh.Makamba sio mtu mwingine.Ninaomba sana mumwite kwenye vikao vya CCM iliawajibishwe.Istoshe akapimwe kichwa pegine anaugonjwa wa akili.

    ReplyDelete