Na Nicodemus Ikonko, Arusha.
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imenunua mashine maalumu zitakazosaidia kuongeza kasi ya kuweka silaha, magari na vifaa vya kuhifadhi takwimu katika nchi tano wanachama wa
jumuiya hiyo.
Nchi wananchama wa EAC ni pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.
Mashine, magari na vifaa hivyo vitakadhiwa kwa jumuiya hiyo katika sherehe fupi itakayofanyika eneo la kuegesha magari la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha
(AICC), Novemba 30, mwaka huu.
Katika sherehe hiyo pia itaonyeshwa shughuli fupi ya kuweka alama kwenye silaha ndogondogo zikiwemo bunduki na bastola.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Bi. Beatrice Kiraso, vifaa hivyo vitasaidia kuongeza kasi ya kufikia lengo la kuweka
alama kwenye silaha ndogondogo zote zilizopo kwenye nchi wananchama ifikapo mwishoni mwa Desemba, 2011, kama ilivyopangwa na mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 740 vimenunuliwa kwa msaada wa Umoja wa Ulaya (EU).
Makabidhiano hayo kwa mujibu wa Mtaalamu wa Silaha Ndogondogo wa EAC, Bw. Leonard Onyonyi yatahudhuriwa pia na mawaziri wa EAC wanaohusika na masuala ya ulinzi,
usalama,mambo ya ndani na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment