07 September 2012

Waziri: Kasi ya kupunguza umaskini haijanirishisha


Na Benedict Kaguo

WAZIRI wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, amesema kasi ya kupunguza umaskini nchini katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, haijamrishisha badala yake imepungua kwa asimilia 2.1 na waathirika wakubwa ni wakulima waliopo vijijini.

Dkt. Mgimwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya kuzindua Mpango wa Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini nchini (MKUKUTA) awamu ya pili ambao ulikwenda sambamba na uzinduzi wa Mkakati wa Mawasiliano.

Alisema zaidi ya Watanzania asilimia 75 ni wakulima waishio vijijini ambao uchumi wao hutegemea zaidi kilimo wakati kasi ya ukuaji wa sekta hiyo hairidhishi.

Aliongeza kuwa, kilimo kinakua kwa asilimia 4.3 hivyo uchumi wao unakua kwa asilimia ndogo ambayo haiwagusi wakulima wengi.

Dkt. Mgimwa pia alizindua Ripoti ya Hali ya Umaskini na Maendeleo ya Watu na kusisitiza kuwa, kukua kwa sekta ya kilimo na kuboreshwa miundombinu vijijini, kutasaidia uchumi kukua na kupunguza umaskini nchini.

Aliongeza kuwa hatua ambazo zimechukuliwa na Serikali kukuza uchumi na kupunguza umaskini ni kutambua mahitaji ya wakulima, kuboresha sera za kilimo na miundombinu ili ukuaji huo uwaguse wananchi wengi walio vijijini.

Alisema kuzinduliwa kwa mikakati hiyo, kutasaidia kuboresha masoko na kuanzishwa viwandwa ili kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa na wakulima.

“Hivi sasa MKUKUTA utashirikisha wananchi ili waweze kushiriki, kuchambua na kutathmini hali ya uchumi,” alisema

1 comment:

  1. Mbona simwelewi huyu mwandishi Benedict Kaguo? Neno "kurithisha" katika habari hii ni kufanyaje?
    Nashauri gazeti kuhakikisha habari zao zinapitiwa na "Proof Readers" kabla hazijachapwa vinginevyo ni aibu kwa gazeti! Binafsi naamini mwandishi ameathirika na lugha yake ya kienyeji na amechanganya neno kuridhika na kurithisha.

    ReplyDelete