24 July 2012
Soko la uhakika changamoto kilimo cha matunda nchini
Na Daniel Samson
SHAMBA darasa ni mbinu ya kuandaa utaalamu katika kata na kijiji, miongoni mwa wakulima kwa kutumia ujuzi unaopatikana kupitia mafunzo shirikishi ili kuongeza uzalishaji.
Pia, imesaidia kuwapatia wakulima mbinu za kilimo bora kwa kufuata mfano wa wataalamu wa kilimo wakitumia zao maalumu.
Ni dhahiri kwamba katika jamii zetu tuna makundi ya watu tofauti ambao hutokana na kazi wanazozifanya, wapo watu ambao
katika jamii hawapendi kufanya kazi mpaka wahamasishwe au wapate matatizo yatakayo watakayowasukuma kufanya kazi.
Wapo watu ambao wao kufanya kazi ni wajibu wao na hawana sababu ya msingi kukataa kufanya kazi, wengine husubiri kusimamiwa au wakati mwingine lazima mjeredi utumike ili waweze kufanya kazi.
Kutokana na uwepo wa makundi hayo lazima tujue kutakuwepo na watu watakaojituma kufanya kazi na kuwa wakombozi wa wale wasioweza kufanya kazi na baadaye wanabaki kuwa soko kwa wale wanaopenda kufanya kazi.
Licha ya usemi wa kilimo ni uti wa mgongo kwa watanzania wengi bado kuna kusuasua kwa sera na utekelezaji wa mipango na mikakati inayohusu kilimo.
Ni wazi kwamba asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima na wengi wanaishi vijijini ambako kuna miundombinu
mibovu na kukosekana kwa soko la bidhaa.
Hata hivyo wapo wakulima wanaolima kwa sababu ya njaa tu na wengine kwa chakula na biashara, pia wapo ambao wamekata
tamaa hivyo wanalima kwa sababu ya kudumisha utamaduni wao, watu hawa wanalima bila kuzingatia kanuni za kilimo, pembejeo na aina ya mbegu.
Mzee Dickson Mwahalennde ni mfano wa kuigwa katika kauli mbiu ya kilimo kwanza kwa wakazi wa Ilomba na watanzania wote, ukifika kwake utaona msitu wa matunda ya kila aina huku mengine ukishindwa kuyatambua kwa majina yake.
Mzee Dickson ni mkulima wa matunda na mboga mboga katika kijiji cha Ilombo kilichopo katika kata ya Ilembo tarafa ya Isangati wilaya ya mbeya vijijini.
Katika bustani yake analima matunda mchanganyiko yakiwemo, parachichi, matunda damu, migomba, matunda mengine majina yake yanaendena na wataalamu waliogundua kwa mfano anna, Godfrey (kutoka Afrika Kusini)na mboga za kila aina.
Historia inaonyesha kuwa, aliaanza kilimo cha matunda miaka ya 1950 akiwa kijana ili kujipatia kipato na kusaidia jamii.
"Nilianza kulima matunda katika umri mdogo hii ni kutokana na kwamba nilikuwa na hamu na shauku ya kuwa mkulima bora na kila tunda ninaloliona kwa wengine nilitamani niwe
nalo nyumbani na ndiyo chanzo cha mimi kujikita kwenye kilimo ninachokishuhudia leo hii," anasema.
Anasema, hakuna kitu muhimu kama kilimo duniani kwani hakuna jamii yoyote inayoweza kuishi bila chakula na chakula ni misingi wa uhai wa mwanadamu hivyo lazima jamii na taifa iangalia njia mbadala ya kuhakikisha kuwa linatiliwa mkazo ili kujikwamua kimaisha.
Anasema siku zote maandalizi ya maisha hufanywa katika
uwekezaji na hapa lazima uangalia ni njia gani inatumika na uwekezaji gani unaufanya.
"Kwa mtu atakayewekeza katika kilimo cha matunda nina
uhakika ataishi miaka yote pasipo kusumbuliwa na njaa au fedha kwani maisha ya mwanadamu hupitia katika hatua
mbalimbali ambazo ni utoto, ujana, kuelekea ujana ,utu uzima na uzee,".
Katika hatua hizi binadamu anakuwa na mahitaji ya chakula, mavazi na malazi, ambapo vyote hivi vinahitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Lakini siyo bora kazi ila kazi ya kilimo cha matunda ambayo ni urithi wa milele kwa familia na jamii kwa ujumla.
Falsafa ya mzee inatufundisha kujitahidi kujiwekeza kabla ya
kusubiri uzeeni ambapo katika kipindi hiki huwezi kufanya kazi yoyote zaidi ya kuwa tegemezi.
Anasema kufafanua kwamba kipindi kigumu katika hatua za
maisha ya binadamu ni uzeeni kwani kipindi hiki unakuwa huna nguvu za kufanya kazi na badala yake unabaki muda wa kula mali ulizowekeza kipindi cha ujana ambapo kama mtu(mzee) hakujiwekeza hawezi kuishi maisha mazuri na baadaye unaweza kuwa ombaomba.
"Kama uliwekeza katika kilimo cha matunda utaendelea kunufaika milele yote na hata wajukuu watarithi kwani kina faida kubwa licha ya kukuingizia kipato pia utapata mboga, chakula, kinywaji kitokanacho na matunda utapata kulinda mwili usishambuliwe na magonjwa kwa kula matunda," anasema Bw.Mwahalende.
Anasema wazee wanatakiwa kuondokana na dhana ya kopatiwa msaasa bali wajishughulishe katika kilimo kama wana nguzu za kusimamia.
Anasema, amekuwa akipata wageni wengi wenye lengo la kujifunza kilimo hicho ambapo huwasadia bure.
"Siri ya kuishi miaka mingi ni kutokana na kula vyakula
vya asili na matunda, vyakula vya viwandani ni hatari kwa afya za watumiaji," anasema
Anasema, baada ya kujifunza kutoka kwa watalaamu
imemsaidia kuendelea kuishi bila kushambuliwa na magonjwa
kutokana na kilimo cha matunda pia, amebahatika kwenda maeneo mbali mbali kwa msaada wa mashirika na watu binafsi kujifunza zaidi.
Kilio changu kikubwa kwa serikali na jamii ni kwamba lazima jamii yetu ijifunze kutoka kwa Bw. Mwahalende kwani namuona kama mkulima wa mfano kwa wakulima wenye lengo la kujiongezea kipato.
Pia serikali kupitia wizara na viongozi wa sekta za kilimo waangalie namna ya kumwezesha mkulima wa kijijini ili
aweze kupata barabara nzuri zinazopitika msimu mzima wa mwaka, kadhalika soko la bidhaa za wakulima wa vijijini ziangaliwe kwa jicho la kuwanufaisha ili kuondoka na utabaka uliopo katika vipaumbele katika sekta zetu.
Bw. mwahelende anawataka wananchi kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kwani kutekeleza wajibu wake pasipo kulaumu mtu yeyote kwani maisha ya mtu yako mikononi mwa mtu
mwenyewe na siyo mtu mwingine.
Pia, anasema wataalamu wa kilimo wasikae ofisini badala yake wazunguke mashambani kuwasaida wakulima ili kuboresha
kilimo chetu na kuondokana nahali duni.
Anasema tangia aanze kilimo hicho ameshuhudia bwana shamba mmoja aliyefika kubadilishana mawazo.
Kama jamii itapenda kubadilika lazima iwe tayari kujifunza
kutoka kwa wale wanaofanya vizuri katika shughuli au utalaamu fulani. Siku zote mtu asiyependa kujifunza hawezi kuendelea na badala yake ataendelea kuwa duni kwa kushindwa kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa na kufanya vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment