20 June 2012
Vodacom yazindua vifurushi vipya vya intaneti
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Mawasilino ya Vodacom Tanzania, imezindua vifurushi vipya vya intaneti ambavyo vitawawezesha wateja wake kupata huduma ya intaneti kwa shilingi 250 kwa siku.
Huduma hiyo ya 'Wajanja Intanet' imeboreshwa zaidi ili kuwawezesha wateja kuelewa huduma za intaneti na kuchagua kikamilifu huduma zitakazowafaa hivyo kuweza kuperuzi na kupata taarifa kwa kasi na kwa bei nafuu kupitia mtandao wa Vodacom.
Hata hivyo, Vodacom ilisisitiza kuwa huduma ya kuperuzi facebook na twitter zitaendelea kuwa bure kwa wateja wote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema kuwa kampuni hiyo imerahisisha huduma hiyo kwa wateja wake ili kuwawezesha kuelewa kiasi ambacho wanatumia katika huduma za intaneti, suala ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa watumiaji wa intaneti kote nchini.
Alibainisha kuwa Kampuni hiyo imeona umuhimu wa watoa huduma za mawasiliano kama Vodacom kuondoa utata ambao unawazuia wateja kutumia mfumo mpya wa teknolojia ya intaneti katika mawasiliano.
“Tumeiweka huduma yetu katika njia ambayo ni rahisi kwa wateja wetu kuelewa kwani tunaamini kuwa hii ni njia rahisi ya kuongeza matumizi ya intaneti katika kueboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Wateja wote wa malipo ya baada au ya kabla watapata huduma ya interneti kwa kasi kupitia simu zao za mkononi na modem.
Aliendelea kusema kuwa kutokana na huduma hiyo mpya, sasa Wateja wa Vodacom watapata huduma isiyo na kikomo na yenye kasi kwa siku saba mfululizo kwa Sh. 10,000 au Sh. 30,000 kwa siku thelathini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment