28 June 2012
Mbunge: CCM wanataka kuniua *Ushahidi wa majina yao kuwasilishwa bungeni
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Ilemela, mkoani Mwanza, Bw. Highness Kiwia (CHADEMA), amefichua mpango wa kutaka kumuua unaofanywa na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jimboni humo.
Bw. Kiwia aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akichangia hotuba ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda.
Alisema watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM, walimvamia na kumshambulia kwa mapanga kichwani.
Hata hivyo, Bi. Kiwia alisema huo ni mpango wa muda mrefu ambao ulipangwa na kusisitiza kuwa, madadiliko katika jiji la Mwanza hayawezi kuzimwa kwa kumuua yeye.
“Hata nikifa leo, wananchi wa Mwanza wataendeleza harakati za kudai mabadiliko, mimi sio kuku wa Krismasi ambao huchinjwa hovyo,” alisema Bw. Kiwia.
Kauli hiyo iliyomfanya Mnadhimu wa shughuli za bunge, Bw William Lukuvi, kuomba mwongozo wa Spika na kusema kuwa, kitendo cha Bw. Kiwia kusema watu waliotaka kumuua ni wafuasi wa CCM wa Ilelema na mpango huo bado upo ni vyema akatoa ushahidi wa wafuasi hao.
Pia Bw. Lukuvi alimwomba Spika kumtaka Bw. Kiwia awataje watu wanaotaka kumuua ili Serikali iweze kulinda maisha yake kwani ni haki ya kila raia kulindwa anapotakiwa kuuwawa.
Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, alimtaka Bw. Kiwia kutoa uthibitisho wa madai hayo ambapo mbunge huyo alisema, siku ya tukio la kupigwa mapanga na kunusurika kufa, katika eneo hilo lilionekana gari la Mbunge wa Viti Maalum mkoani humo Bi. Maria Hewa (CCM), ambayo inathibitisha kuwa wafuasi wa chama hicho walihusika kutaka kumuua.
Baada ya kumtaja Bi. Hewa, Spika alimba Bw. Kiwia siku saba awe amewasilisha ushahidi na majina ya watu waliotaka kumuua ili waweze kuchukulia hatua stahiki kwa mujibu wa sheria
“Nipo tayari kutoa ushahidi wote na majina ya watu wanaotaka kuniua, nitayawasilisha bungeni kwa muda niliopewa,” alisema.
Bw. Kiwia alishangazwa na namna Serikali inavyoendesha mambo yake ambapo tukio la kutekwa kwa Kiongozi wa Madaktari Dkt. Steven Ulimboka ni jambo la kusikitisha.
Alisema lazima Serikali iwe macho na vitendo vinavyoweza kutafsiriwa kuwa vinakandamiza wananchi wanaodai mabadiliko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
TUSIFANYE MASIARA USHAHIDI NI MGUMU HIVI CHADEMA NI LAZIMA KUTUMIA NGUVU SANA KUTOA HOJA NA PIA KUTUKANA MBONA WANAMTATA MUNGU GANI??? NI MUNGU KWELI AU FREEMASON SASA HIVI WALA HAKUNA PEOPLES POWER UNAFIKI MKUBWA HANGANYIKI MTU MUNACHOTAKA NI MADARAKA TU WALA SIO KUTETEA WANYONGE SHINDWENI MULEGEE
ReplyDeleteCHADEMA MBA TU....MMEONA WATANZANIA NI WAJINGA KIASI HICHO, NYIE NI KUZSHA NA KULIA KILA SIKU ...WASENGE
ReplyDeleteNAIOMBEA TANZANIA MPINZUZI YA KIJESHI....HAWA WANASIASA WOTE MBWA TU SI CCCM WALA CHADEMA...MBWEHA WAKUBWA
ReplyDeleteTanzania inabidi tuchinjane kwanza heshima hakuna , mimi nabariki mapinduzi ya ncha ya upanga DAMU INABIDI IMWAGIKE ....Ulimboka kamwaga yake TEYARI......
ReplyDelete