PICHA NO 2 mtoto Gadson Gamasoni akiwa amelala kitandani - nyumbani kwao Nazareth
Na Mwajabu Kigaza
ELIMU ni msingi wa maisha katika kila jamii, pia ni urithi pekee wenye manufaa makubwa kwa watoto na jamii kwa ujumla.
Pamoja na jitihada za serikali katika kufanikisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu yaliyofikiwa nchini, bado jamii kubwa haijaona umuhimu wa kutumia fursa hiyo katika kuwapatia watoto wao elimu hiyo kikamilifu.
Hatua hii imekuwa ikichukuliwa kwa namna tofauti na jamii kutokana na wengine kutokuwa na msimamo wa kuwapatia elimu watoto wao.
Baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wamekuwa wakiwazuia watoto wao kusoma na kuwatwisha majukumu yao ya kutafuta kipato hivyo kuwaingiza katika shughuli mbalimbali za kukuza uchumi wa familia.
Mbali na kuwepo kwa kipato duni lakini hali hii kwa jamii zingine imeonekana kuwa kinyume ambapo hushindwa kuwapatia elimu watoto wao kutokana na matatizo ya ugonjwa kama ilivyotokea kwa Mtoto Gadson Gamasoni.
Wazazi wa Gamasoni wanatambua umuhimu wa elimu kwa kuamini kwamba, kumpatia elimu mtoto ni kumuondoa katika ujinga.
Pamoja na kuamini hivyo, bado matumani yao yaligonga mwamba baada ya mtoto huyo kukutwa na tatizo la ugonjwa unaomsumbua kwa miaka tisa.
Bw. Gamasoni mwenye umri wa miaka 21 ni Mkazi wa Nazareth katika Manispaa ya Ujiji, Kigoma ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia ya Bw. Gamasoni Kisodya yenye jumla ya watoto watatu.
Bw. Gamasoni alipata tatizo hilo akiwa Darasa la Tatu mwaka 2003 baada ya kuanguka kutoka juu ya mti wa mwembe uliopo eneo la Shule ya Msingi Katubuka katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji.
Baada ya kuanguka akiwa na wenzake, wazazi walianza matibabu ambapo alikuwa amejeruhiwa zaidi eneo la miguu yote sambamba na kiuno ambapo kwa hatua za awali walimpeleka katika Hosiptali ya Mkoa wa Kigoma-Maweni ambapo alilazwa kwa zaidi ya mwaka.
Kwa nyakati tofuati alilazwa katika Hosiptali za Nyamasofu wilayani Kasulu na Moi-Muhimbili ambapo hadi sasa ili kunusuru maisha yake amerudishwa Muhimbili.
Bw. Gamasoni amesumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu bila mafanikio ambapo mbali na matatizo ya ulemavu ambayo hayatapona, lakini tatizo linalompa shida ni kutokwa ovyo kwa haja kubwa na ndogo bila kujizuia hali ambayo inaweza kupatiwa ufumbuzi India.
Mbali na kusumbuliwa na hali hiyo anaelezwa kuwa ni miongozi mwa wanafunzi walio na kipaji cha pekee kwani kwa muda wote nyumbani pamoja na kuwa na tatizo hilo, amekuwa akijishughulisha na mambo ya ufundi wa vifaa vya umeme kama kutenganeza Redio, televisheni, Deki na simu ikiwa ni pamoja na kuunda kifaa cha kurushia miziki FM 100 katika eneo la Nazareth.
“Nimeamua kujiendeleza ili kukuza kipaji changu ambacho nilijaliwa na Mungu, naimani kuwa endepo ningefanikiwa kupata elimu ni wazi kuwa kipaji hiki ningeweza kukitumia vizuri natamani sana kupata elimu,” anasema.
Baba wa Bw. Gamasoni anaishi eneo la Nazareth akiwa ni mfanyabiashara wa kawaida na akiwa ambaye anauza kanda za nyimbo za muziki ya injili na amekuwa akitumia fursa hiyo kumtibisha mtoto huyo kwa zaidi ya miaka minane sasa bila mafanikio ambapo anasema sasa ameishiwa hivyo kuhitaji msaada.
Anasema, amekuwa akisaidiana mke wake katika kuhakikisha mtoto huyo anapata malezi na mambo yote yanayomstahili na wamekuwa wakitumia muda mwingi wa kazi kufuatilia matibabu ya mtoto hivyo wakati mwingine shughuli za uzalishaji mali kukwama.
Alisema kuwa, kipindi chote hicho Bw. Gamasoni alianza kupooza mguu moja na baada ya muda wa wiki mguu mwingine nao ulipooza, pamoja na jitihada za matibabu mbalimbali inaonekana kuwa mtoto wangu atakuwa mlemavu katika maisha yote.
“Tatio hili la kupooza limesababisha kijana wangu kushindwa kujizuia haja ndogo na kubwa, ikiwa ni pamoja na kutokwa na madonda katika eneo la makalio ambayo hayaponi kwa takribani miaka minane sasa kwani hainuki wala kukaa haja zote ni hapohapo,” alisema.
Alilazwa kwenye kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) ambako alitibiwa kwa takribani miaka miwili bila ya mafanikio yoyote ambapo aliendelea kupooza.
Hatua hii ilionekana mara baada ya kupata ufadhili kutoka katika Hospitali ya Muhimbili ya kumsomesha hivyo alilazimika kuvaa pampasi ili kumsaidia kutokana na haja kumtoka bila kujua.
Baada ya uchunguzi iligundulika kuwa nyama zimeoza na mfupa kuanza kutafunwa na wadudu hivyo kusababisha donda kubwa ambalo lilikuwa likitoa usaha, alifanyiwa uparesheni lakini bado madonda hayo yaliendelea na kusababisha kutoendelea na masomo.
Uongozi huo uliamua kumpatia elimu hiyo kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kielimu, na hivyo kumpeleka katika shule ya walemavu ili aweze kupata elimu zaidi na kukuza kipaji chake.
“Tatizo hili lilisababisha turudi nyumbani ambapo ilibidi nipatiwe elimu ya wiki moja jinsi ya kumtunza mtoto, maji ya kumsafishia madonda ni maji ya drip na dawa na kumfungia ni asali ambapo huo ndio ushauri wa daktari,” anasema.
Kutokana na tatizo hili Dkt. Nungu wa Hospitali ya Muhimbili ambaye alikuwa akimtibu aliweza kufanya mawasiliano na madaktari waliopo nchini India ili kuweza kutatua tatizo la kutokwa na haja zote bila kujua.
“Niliweza kufanyia kazi ushauri wake na kuanza kuomba misaada kwa watu mbalimbali ambapo walijitokeza watu kusaidia michango yao ya hali na mali ili kuwea kunusuru maisha ya mtoto wangu,” anasema.
Kutokana na umuhimu wa jambo hilo baadhi ya wafanyabishara, ndugu na jamaa wameunda kamati ya kukusanya michango kutokea Mkoa Kigoma kwa ajili yamatibabu ya kijana huyo inchini India ikiwa ni pamoja na vikao vya kifamilia.
Harambee zilifanywa na wakazi wa mkoa Kigoma katika kukusanya fedha za matibabu sh. milioni tisa zilipatikana mpaka sasa.
Kwa hatua ya kuanzia inatakiwa jumla ya sh. milioni 13 kwa ajili ya gharama za matibabu ya kijana huyo nchini India na matiababu yalitakiwa kufanyika kuanzia 2010.
Bw. Mifuro Mpozemenya ambaye pia ni miongoni mwa watu waliogoswa walianzisha kamati rasmi kukusanya fedha kwa watu waliotoa ahadi katika harambee iliyofanyika katika Manipsaa ya Kigoma Ujiji ambapo katika harambee hiyo jumla ya ahadi ilikuwa ni sh. milioni saba ambapo baada ya ufuatiliaji sh. million sita zilipatikana.
“Sio siri nimeguswa sana kuamua kumsaidia kupitia NMB akaunti 5161605656, nawaomba Watanzania wote na wadau mbalimbali waguswe katika kumsaidia mtoto huyo tusikalie kuchangia harusi na masherehe mengine hata matatizo pia watu wajitokeze kuchangia ili kuokoa maisha ya mtoto huyu,” anasema Bw. Mpoemenya.
No comments:
Post a Comment