26 October 2011

Gaddafi azikwa usiku jangwani

*Mazishi yafanywa siri kama Osama Bin Laden

TRIPOLI, Libya

MWILI wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, mwanawe Muatassim na Mkuu wake wa Majeshi, Abu Bakr Younis Jabr imezikwa
katika kaburi la siri lilopo jangwani jana alfajiri.

Ofisa mmoja mwandamizi kutoka Baraza la Taifa la Mpito nchini humo (NTC) alilieleza Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana kuwa miili hiyo imezikwa katika kaburi la siri ambalo ni vigumu kutambulika na wananchi.

Mazishi hayo yamefanyika zikiwa zimepita siku tano kadhaa, huku watu wakiendelea kuhoji utawala mpya ulikuwa na mikakati gani juu ya miili hiyo.

Awali, familia ya Gaddafi iliyopo uhamishoni nchini Algeria ilipendekeza ikabidhiwe mwili wa kiongozi huyo na uzikwe katika mji wake alikozaliwa wa Sirte.

Msemaji wa NTC mjini London, Guma al-Gamaty alilieleza BBC kwamba mazishi tayari yalikuwa yamefanyika usiku wa kuamkia jana.

Mwandishi wa Shirika la Habari la Associated Press alisema kuwa alipokea ujumbe mfupi kutoka kwa ofisa mmoja wa kijeshi mjini Misrata, Bw. Ibrahim Beitalmal, ukieleza kwamba:

"Mazishi yamefanyika katika eneo la siri majira ya saa 11:00 saa za Libya (saa 9:00 Afrika Mashariki), baadhi tu ya ndugu na maofisa waliweza kuudhuria na kuombea miili hiyo."

Ofisa mwingine wa baraza hilo awali alilieleza Shirika la Habari la Reuters kwamba Kanali Gaddafi mazishi yake yangefanywa katika utaratibu wa kawaida kwa kuwashirikisha mashehe kadhaa.

"Ni eneo ambalo halifahamiki ndani ya jangwa," alisema na kuongeza mazishi yalipaswa yafanyike kwa sababu miili hiyo ilikuwa imefikia hatua mbaya ambayo haipaswi kuachwa tu," aliongeza.

Mashuhuda walisema kuwa miili hiyo mitatu ya Kanali Gaddafi, mwanawew. Muatassim na Mkuu wa majeshi iliondolewa usiku katika jokofu ambalo walikuwa wamehifadhiwa mjini Misrata na kupelekwa eneo la mazishi.

Kwa mujibu wa BBC sala ya pamoja ilifanyikia katika eneo hilo kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa kusikojulikana.

"Kazi yetu imekamilika," mlinzi mmoja katika eneo hilo, Salem al Mohandes, aliieleza Television ya Kiarabu ya Aljazeera. Yeye (Gaddafi) aliondolewa katika eneo hili la Misrata na askari, walimpeleka kusikojulikana kumzika, hivyo sitambuhi kama wamemzika kweli au hapana," aliongeza.

Mwakilishi wa BBC mjini Tripoli, Katya Adler alisema kuwa maswali mengi yalikuwa yanawakabili viongozi wa utawala mpya wa Libya juu ya hatima yake baada ya kukaa kwa zaidi ya siku nne pasipokutoa uamuzi wowote.

"Tamaduni za waislamu mara baada ya mtu kufariki dunia basi ni lazima taratibu za mazishi zinapaswa kutochukua muda kama ilivyotokea kwa Kanali Gaddafi;

"Lakini vinongozi wa NTC walisema kama watanuruhusu kaburi la Kanali Gaddafi kuonekana wazi wazi litatoa nafasi kwa baadhi ya wananchi pamoja na wafuasi wake kufanya matambiko, kitu ambacho wanaona siyo sahihi," aliongeza.

Hatua kama hiyo ilichukuliwa na Serikali ya Marekani kwa alipouawa Kiongozi wa Kigaidi wa al Qaeda, Osama Bin Laden, Mei mwaka huu ambaye mwili wake ulitupwa baharini, lengo likiwa ni kuzia wafuasi wake kulifanya kaburi lake sehemu ya matambiko na kuwaongezea hasira dhidi ya waliomuua.

Viongozi wa Baraza la Taifa la Mpito (NTC) wameendelea kusisitiza kwamba Kanali Gaddafi aliuawa katika majibishano ya risasi kati ya wapiganaji wa baraza hilo na wafuasi wa kiongozi huyo baada ya kumkamata katika karavati.

Baadhi ya wanachama wa baraza hilo pamoja na Jumuiya za Kimataifa wamekuwa wameonesha hisia tofauti juu ya tukio hilo la mauaji kwa ujumla.

Marekani, Uingereza na Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu ya Kimataifa wamekuwa wakishinikiza uchunguzi ufanyike juu ya namna ambavyo mauaji ya Kanali Gaddafi yalivyotokea, kiongozi mmoja wa NTC alisema kuwa Kanali Gaddafi huenda aliuawa na wafuasi wake wenyewe kwa lengo la kukwepa lawama ambazo zigeweza kutokea baadaye.

Alivyokamatwa kisha kuuawa

Saa za asubuhi alhamisi iliyopita, Kanali Gaddafi akiambatana na wafuasi wake watiifu, aliamua kulikimbia eneo ambalo lilikuwa ngome yake iliyosalia, akiwa na msafara wake wa magari 75.

Majira ya saa 8:30 ndege ya kijeshi za Ufaransa zilizokuwa katika kundi la NATO
ilishambulia msafara huo uliokuwa unakimbia kutoka mji wa Sirte kwa mwendo kasi, kama kilometa 3-4 magharibi mwa mji huo.

Pamoja naye, katika msafara huo walikuwamo mtoto wa kiongozi huyo, Mutassim, Mkuu wake wa majeshi, Abu Bakr Younis Jabr na wote baadaye waliripotiwa waliuawa.

Taarifa za NATO baadaye zilisema kuwa shambulio la kwanza liliharibu gari moja na kusababisha msafara kugawanyika katika vikundi kadhaa.

Moja ya makundi hayo, ambamo Gaddafi alikuwa lilielekea kusini ambako lilishambuliwa tena na wapiganaji wa NATO, safari hii magari 11 yakaharibiwa.

Baada ya shambulio hilo, Gaddafi na wafuasi wake wachache walifanikiwa kutoroka na kukimbia kwa miguu na kwenda kujificha katika karavati lililokuwa limejaa takataka, ndipo wapiganaji wa waasi walifika na kumkamata.

Mmoja wa wapiganaji hao, Salem Bakeer alilieleza Shirika la Habari za Uingereza, Reuters mwanzoni waliwashambulia kwa makombora ya kutungulia ndege, lakini haikusaidia.

"Baadaye, tuliwafuata kwa mguu, mmoja wa wafuasi wa gaddafi alitoka akipunga mkono wenye bunduki hewani. Aliponiona tu akaanza kurusha risasi upande wangu, nadhani gaddafi aliwaeleza kuacha, mara akaanza kusema, mkuu wangu yuko hapa, mkuu wangu yuko hapa', 'Muammar Gaddafi yuko hapa amejeruhiwa'.

Gaddafi akamatwa

Kanali Gaddafi hatimaye alikamatwa mchana, na Salem Bakeer aliieleza Reuters: "Tuliingia ndani na kumtoa Gaddafi nje. Alikuwa anahoji 'tatizo nini?, tatizo nini? Kitu gani kinaendelea? Tulimchukua na kumpakia kwenye gari. Mmoja wa wapiganaji hao aliwaonesha waandishi wa habari bastola ya dhahabu, aliyosema aliichukua kwa Gaddafi.

Baadaye mwili wa kiongozi huyo ulioneshwa akiwa ameshapigwa risasi kichwani, jambo ambalo limeacha maswali kama ameuawa na waasi waliomkamata ay aliuawa na walinzi wake.
BBC/ALJAZEERA

6 comments:

  1. Wanaona haya hawa, wamemuua bure mtu huyu. SAW anajua hilo vema. NTC imemuua, wahirika wa Marekani na wengineo wamefurahi, nao wao zao zina hesabiwa na Allah. Mafuta yake na utajiri wake waliuonea gere. Mungu yupo.

    ReplyDelete
  2. mwisho wa yote ni maut hivyo Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Pepon Ameen

    ReplyDelete
  3. Wakoloni ni watu wabaya sana utajiri wa Libya ndio umewafanya wamuuwe GADAFI; Ila kitu kinamwanzo na mwisho itafikia wakati na sisi WAAFRICA tutasema kunyanyaswa basi; MUNGU ATATUSAIDI TUEPUKANE NA MADHALIMU HAWA.

    ReplyDelete
  4. lakini jamani embu tuludi nyuma, huyu mshkaji ni tajiri sana tena mno, kwanini hakusoma nyakati mapema na kukimbia nchi yake na kula hizo pesa na familia yake, uraisi ndo huyo umempata sasa, pesa nyingi ameziacha na utajiri mkubwa sana. amefanya nini? nguvu ya uma ni kubwa sana hivyo tz ijifunze kupitia hili.

    ReplyDelete
  5. Atakae makuu huvunjika mguu, kwa Gadafi umeme bure,maji bure, afya bure na huduma muhimu zote bure,sasa wananchi wa libya wanataka nini zaidi ya hayo,ngoja waone sasa kilichomtoa kanga manyoya kwa kusikiliza unafiki wa magharibi

    ReplyDelete
  6. bwana wewe usiwe mjinga kwani wewe ukimchukua nduguyo kijijini na kumleta dara huko mbezi ktk hekalu lako na kumpangia masharti na kumnyanyasa unadhani atapenda kuishi ktk hiyo nyumba yako kubwa sasa huo mfano ni sawa na walibya wanayajua yote hayo wameyaona lakini kuma mambo huyo mzee wananchi hawakuyapenda kama alikuwa mzuri kwa nini siku ya kwanza aliwaita wananchi anaowatawala mapanya huwezi jiuliza hilo acha hizo hujui dunia inakwendaje angalia ya kwako tanzania yanayokusibu wakipata taabu wao raha za kwao wewe hayakuhusu bwana ujinga wake kauwawa kama wmizi wa kariokoo tena mwizi wa simu mtu alikuwa tajiri kuliko kuna usemi unasema mwogope mungu waheshimu binadamu binadamu wenzio wana nguvu zaidi kuliko mungu hao mapanya wamemwua tayari pesa ilifanya nini hao aliowapa pesa walimkimbia

    ReplyDelete