25 July 2011

Stella awa Redd's Miss Kinondoni 2011

Na Victor Mkumbo

MNYANGE Stela Mbuge, juzi alitawazwa kuwa Redd's Miss Kinondoni, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Mlimani City, Dar es Salaam.

Stela aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wenzake 11 baada ya kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa na Miss Tanzania wa mwaka 2007, Richa Adhia.

Fainali za Redd's Miss Kinondoni zilihudhuriwa na umati wa mashabiki wa sanaa hiyo ambapo pia ilipambwa na burudani mbalimbali.

Burudani zilizokuwepo katika fainali za Redd's Miss Kinondoni, ni pamoja na bendi ya THT, Mataluma, sarakasi kutoka katika kikundi cha Mama Africa, na shoo iliooneshwa na washiriki walioingia katika tano bora ya Miss Tallent.

Stela aliibuka kidedea katika mashindano ya Redd's Miss Kinondoni na kuzawadiwa sh. milioni mbili pamoja na televisheni aina ya LCD iliyounganishwa na king'amuzi cha Star Times chenye ya sh. milioni moja.

Mshindi wa pili alikuwa Husna Maulid ambaye alizawadiwa sh. milioni 1.5 na televisheni iliyounganishwa na king'amuzi cha Star Times, wa tatu ni Hamisa Hassan ambaye alizawadiwa sh. milioni 1.5 na televisheni iliyounganishwa na king'amuzi.

Mshindi wa nne Fatma Pongwa na watano ni Felister Philip ambao kila mmoja alizawadiwa sh. milioni moja.

Washiriki walioshika nafasi ya sita mpaka ya 10 walizawadiwa sh. 500,000 wakati waliobakia walipewa kifuta jasho cha sh. 300,000 kila mmoja.

Mshindi wa taji la Miss Talent katika mashindanoha hayo ni Fatma Pongwa ambaye alipata sh. 200,000 pamoja na televisheni, balozi wa Giraffe ni Hamisa Hassan ambaye alipewa sh. milioni moja na mshiriki mwenye nidhamu ni Renalda Apole ambaye alipata sh. sh. milioni moja pamoja na televisheni.

No comments:

Post a Comment