25 July 2011

Khan amsimamisha Judah kwa Ko

LAS VEGAS, Marekani

MPIGANAJI wa England, Amir Khan ameshinda mechi yake nyingine katika uzani wa kilo 63.5 dhidi bondia mkongwe, Zab Judah.Mwingereza huyo alimaliza pambano
katika raundi ya tano katika mechi hiyo ya kuunganisha mataji, alimpiga konde katika mwili, ingawa Judah alidai kuwa,  alikuwa amepigwa chini ya mkanda.

Khan alikuwa akirusha ngumi za maana kabla ya kurusha ngumi  iliyomkalisha Judah chini.

Bondia huyo Mwingereza alifuarahia ushindi wake baada ya raundi ya tano kwa kumtwanga kwa KO, Judah katika pambano la kuunganisha mataji la uzani wa light.

"Kama ingeendelea raundi nyingine chache, ningemtwanga kwa kwa uwazi," alisema Khan.

Khan alitawala mechi wakati aliporusha ngumi ya kulia ambayo ilitua katika mkanda wa Judah,  ambaye alianguka  jukwaani. Judah alipiga magoti huku mwamuzi Vic Drakulich akimhesabia katika dakika 2:47  ya raundi ya tano.

Judah alisimama na kwenda kwenye kona yake, huku Khan na kambi yake ikishangilia. Awali, Judah alilalamika kugongwa kichwa na Khan na alikuwa akitokwa damu puani na kuchanika usoni.

"Ilikuwa ni pigo chini ya mkanda, nilikuwa nikijiweka sawa," Judah alisema. Pale ilikuwa ni kujilinda mwenyewe.

Ushindi huo umemfanya Khan ambaye ni bingwa wa zamani wa Olimpiki azidi kuwa na rekodi nzuri.Hakupata shida sana katika kupigana na mpinzani wake anayetumia mkono wa kushoto, alitumia wepesi wake kumwadhibu kwa ngumi.

"Ninafikiri kasi yangu ilimzidi, sambamba na nguvu zangu," alisema Khan. " Ninafikiri nilikuwa nikimuumiza na ilikuwa ni suala la muda tu kumaliza pambano.

Mwisho wa pambano ulikuja wakati Khan aliporusha ngumi ya kulia ambayo ilikuwa halali, lakini ya wazi. Judah alikwenda chini na kubaki hapo akiwa chali wakati akihesabiwa.

Khan, ambaye rekodi yake imeboreshwa ameshinda mechi 26 na kupoteza moja, huku akishinda 18 kwa knockout, alipigana katika ukumbi ambao aliutumia kumtwanga Marcos Maidana, Desemba mwaka jana.

Khan, Aprili alimtwanga Paul McCloskey katika mechi yake ya mwisho iliyochezwa mjini Manchester.

Judah ana rekosi ya kucheza  mechi 41 na kupigwa saba, katika mechi ya juzi alionekana muda mwingi kujihami zaidi.

Khan katika mechi hiyo alirusha ngumi 284, ambapo 61 zilimpata mpinzani wake, huku Judah akirusha ngumi 115 na 20 ndizo zilimkuta mpinzani wake.

No comments:

Post a Comment