03 February 2011

Naomi akiri alikuwa teja, chapombe

LONDON, Uingereza

MWANAMITINDO Naomi Cambell, amekiri kuwa alikuwa akinywa sana pombe na kutumia dawa za kulevya, baada ya kuwa maarufu.Mwanamitindo
huyo amekiri alikuwa teja wakati alipokuwa na umri wa miaka 20 na alikuwa akipenda starehe usiku na siku iliyofuatia alishindwa kupata usingizi.

Alisema kuwa tabia hiyo ya ulevi na utumiaji wa dawa za kulevya ilimletea matatizo mengi.

Aliiambia GQ, kuwa mbali ya kunywa pombe alikuwa akitumia dawa za kulevya.

Alisema hali hiyo iliathiri upangaji mipango yake na kumletea matatizo mengi na kwamba hakupenda jinsi alivyokuwa.

"Kunywa na dawa za kulevya kwa sasa ni mzigo kwangu na havinifanyi mimi kuwa mtu mzuri."

Mwanamitindo huyo alisema baada ya kugundua tatizo lake aliachana na matumizi ya dawa za kulevya na ulevi kupita kiasi na kisha mambo yake yalikuwa mazuri tena kwa kupata fedha.

Alisema: "Nilikuwa ni msichana na pia nilikuwa nikijirusha usiku wa manane. Ilikuwa ni kwa kutaka kujifurahisha.

Nilikuwa siwezi kutoka kitandani bila ya kupata (dawa za kulevya). Ilikuwa ikinifanya kufikiria cha kufanya. ILikuwa ni kitu cha kujifurahisha na sikujua jinsi ilivyokuwa na nguvu, ilikuwa ni njia mbaya sana.

"Furaha huja na madhara yake. Unajiua mwenyewe… nilikuwa teja kweli.Mzaliwa huyo wa London, mwenye miaka 40 alisema hakuomba msaada wakati alipokuwa kwenye hali hiyo, hadi alipokuja kukaa sawa.

Alisema: "Kurudi katika hali ya kawaida ni kitu kizuri. Hakuna kitu cha kuhofia."Kama unahitaji kusaidiwa, omba usaidiwe, unahitajika katika muda huo kushughulika na hali hiyo. Inabidi uwe na nidhamu hiyo mpya. Jiambie kuwa uko tayari kusema hakuna mashaka.

Alisema kuna watu wengi walitoka katika matatizo hayo, mfano akiwa ni Eric Clapton.

No comments:

Post a Comment