28 January 2011

Majira yazindua kamati kuchochea maendeleo Kagera

Na Theonestina Juma, Bukoba

KAMPUNI ya Business Times kupitia gazeti lake la Majira imezindua kamati ya kuchochea na kufuatilia maendeleo ya Mkoa wa Kagera, ambapo
Bw. Yusto Muchuruza amechaguliwa kuwa mwenyekiti akisaidiwa na Bw. Edward Tibihenda.

Uzinduzi wa kamati hiyo ambayo wajumbe wake waliteuliwa na wakazi wa Kagera wanaoishi Dar es Salaam na kupata Baraka kutoka kwa wakuu wa wilaya za mkoa huo, ulifanyika mjini hapa jana. Wajumbe waliohudhuria mkutano huo walikuwa 11 kati ya 14.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa katika wadhifa huo, Bw. Muchuruza alipongeza mpango ulioanzishwa na Kampuni ya Business Times kwa kuwa unalenga kuchochea maendeleo ya jamii mkoani wa Kagera.

“Kagera ina raslimali nyingi, ikiwemo raslimali watu, kila mwana Kagera angetoa asilimia moja ya mapato yake, Kagera ingezidi Jiji la London,” alisema, Bw. Muchuruza.

Alisema chini ya mwelekeo huo mpya wa Majira uwezekano wa kufaulu upo, na kwamba kinachotakiwa ni kila mmoja kutimiza wajibu wake.

Bw. Muchuruza alisema kati ya wajumbe waliopendekezwa kuunda kamati hiyo hakuna hata mmoja aliye kinyume na mawazo ya Sekretarieti ya Majira ambayo ndiyo inaratibu mpango huo.

 “Mtegemee kuwa jamii nzima itakubali mpango huu… mimi napenda kufanya kazi, tufanye kazi ili tuweze kufanikiwa…hatuendelei
kwa sababu siri ni moja ni kwa kuwa hatufanyi kazi,” alisisitiza Bw. Muchuruzi.

Alitoa mwito kwa wajumbe wa kamati hiyo kuepuka kutekeleza majukumu yao kama wapelelezi. Alishauri mkakati wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo usiwalenge wana-Kagera wanaoishi Dar es Salaam tu bali hata wale waliopo mikoa mingine na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti, Bw. Tibihenda alipongeza Majira kuanzisha mpango huo kwa kuwa mambo mengi yanayofanyika kwenye vijiji vyao hayafahamiki.

Aliahidi kushirikiana na wana-kamati kutekeleza majukumu yatakayokuwa mbele yake ili kazi hiyo iweze kufanyika kikamilifu.

“Tunapaswa kujitahidi ili wale waliotuamini waone kazi imefanyika inavyotakiwa…tuondoke hapa tukionekana tumebeba mzingo mkubwa wa kuponyesha wale waliotuteua,” alisema Bw. Tibihenda.

Awali mwakilishi wa Business Times Ltd, Bw. Arnold Kimanganu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Business Times, Bw. Rashid Mbuguni, alisema dhamira ya maendeleo kwa wana Kagera si jambo kipya, hivyo haziwezi kupotea bali litabaki kuwa deni litakaloendelea kuwazonga wananchi wa Kagera hadi hapo watakapofanikiwa.Alisema chombo cha Majira kitasaidia kuunganisha nguvu za wakazi
wa Kagera.

Alisena itakuwa chachu tu ya kujumuisha mipango na nguvu za ndani na nje ya mkoa, kuhamasisha jamii na kuisaidia kuondoa vikwazo vinavyokwamisha na kurudisha nyuma jitihada za maendeleo.

3 comments:

  1. Hili halijakaa vizuri. Hata kama kampuni hii ni ya wanakagera, inapaswa kuangalia masuala ya kitaifa zaidi. Kama jukumu lenu ni kuelimisha wananchi kwa njia ya habari, mkiingia kwenye kazi za kagera kama kipaombele chenu tutawaona wabaguzi.
    Tatizo la ukabila, ukanda, umkoa, umimi tunalikuza kwa mipango kama hii. Kwa nini kagera tu? kwa nini wilaya yako tu? kwani hii kampuni ni ya watu wa kagera tu? au unatuonyesha nini?

    ReplyDelete
  2. mh!maendeleo yanaletwa bila kujali eneo wala mtu gani kwani kila sehemu watu wanaungana na wanaleta maendeleo hivyo hakuna aja ya kupinga mpango huu kila sehemu inji hii watu wanachangia maendeleo ya watu na maeneo wanayotaka yanaleta ushindani kimaendeleo wala haizuii maendeleoo mengine au pengine au ukabila !Tumeona jana Mrema,Vunjo ,Mbeya kila sehemu wanachangia maendeleo

    ReplyDelete
  3. wewe unaye ogopa watu kuchangisha pesa kwa kabila lao kwasababu unasema italeta ukabila ninafikiri akili yako iko kwenye ile enzi ya ujamm - kila mtu awe maskini. kuchangisha pesa ndio kume wafanya wakenya wengi sana kwenda kusoma america na europe. matokeo yake angalia sasa wakenye walioko abroad wanatuma back home mabilioni ya pesa kusaidia kwao

    ReplyDelete