LONDON, Uingereza
HATIMA ya baadaye ya klabu ya Manchester United, imeingia mashakani baada ya mtu muhimu kwenye klabu hiyo kusema wamiliki wake familia ya Glazer wataiuza.Aliyekwua mtendaji wa Old Trafford, Mike Edelson alisema: "Hakuna siri katika
hilo kwa wakati huu, familia itaiuza klabu."
Inadaiwa kuwa milango imefunguliwa kwa matajiri wa Uarabuni, ambapo familia ya Kifalme ikiongozwa na Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani, inataka kuinunua United kwa bei ya pauni milioni 1.5.
Maoni ya Edelson ni alama ya kwanza kwamba familia ya Glazer, inaweza kusikiliza ofa kwa ajili ya kuiuza United, kutokana na madeni.
Miamba hiyo ya Ligi Kuu England, ina deni baada ya kuinunua kwa pauni milioni 790, miaka mitano na nusu iliyopita familia hiyo inataka kupata faida baada ya kutumia fedha zao.
Chanzo kutoka Man United kilisema kuwa familia ya Glazer, iko tayari kuiuza timu hiyo baada ya kulipa deni pauni milioni 252 kati ya pauni milioni 752 inazodaiwa.
Mtu mmoja wa karibu alisema: "Habari fupi ni kwamba tayari wameshaingiza fedha kutoka kwa upande wa tatu katika kujiandaa kuuza klabu."
Chanzo hicho kililiambia gazeti la SunSport, kwamba Kampuni ya Qatar Holdings inajiandaa kuinunua United wakati utakapowadia.
Kilisema baada ya nchi ya Qatar, kupata wenyeji wa Kombe la Dunia 2022, nchi hiyo inataka kutanua kueleweka kwake katika mchezo huo Duniani."
Mjumbe wa bodi wa United, Edelson amekuwa karibu wa familia ya Glazer, tangu walipoichukua klabu hiyo mwaka 2005.
Alisema hayo wakati akiwa katika kipindi cha maswali na majibu cha Maccabi Sports Club mjini Prestwich, Manchester.
Familia ya kifalme ya Qatar, ina utajiri unaokadiriwa kufikia pauni milioni 40, wiki iliyopita walikuwa wadhamini wa kwanza wa jezi za Barcelona kwa mkataba wa pauni milioni 125.
No comments:
Post a Comment