11 March 2013

Kigogo scania kortini akidaiwa kuiba milioni 177/-


Na Judith Michael

OFISA Utawala wa Kampuni ya Scania (T) Limited tawi la Dar es Salaam, Didier Abdallah Mlawa(38) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kughushi saini ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo na kujipatia kiasi cha sh. Milioni 177

Mtuhumiwa alifikishwa mahakami hapo jana na kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka Bi Ester Martin, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Bi Janeth Minde.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alighushi saini ya mhasibu na Mkurugenzi na wa kampuni hiyo kisha kufungua akaunti benki kwa kutumia nyaraka hizo za uongo.

Mwendesha mashtaka huyo alisema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo kwa makosa mawili ambayo ni kughushi saini na wizi  katika kampuni ya Scania.

Mwendesha mashtaka alisema,mtuhumiwa alifanikiwa kufungua akaunti hiyo kwa kutumia majina ya wafanyakazi wastaafu waliokuwa wanafanya kazi katika kampuni hiyo.

"Mtuhumiwa alifungua akaunti hiyo Januari 10-26,mwaka huu kama mfanyakazi ambapo alifanikiwa kampuni yake kiasi cha shilingi 177.3 mali ya wafanyakazi wenzake"alisema,Mwendesha mashtaka huyo

Mtuhumiwa huyo amerudishwa rumande hadi Machi 20, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.
.....................................


No comments:

Post a Comment