23 August 2011

Diwani avamiwa auawa kikatili

Na Patrick Mabula, Kahama

DIWANI wa CCM Kata ya Bugarama, wilayani Kahama Bw.Peter Kisiminza (50) ameuawa kinyama kwa kukatwa mapanga nyumbani kwake katika Kijiji cha Buyange.Baada ya
kumkata mapanga watu hao waliokuwa wamemvamia usiku wa manane  pia walifanya unyama mwingine kwa kuwabaka watoto wake wawili wa kike na kisha kuiba mali na kutoweka.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa Shinyanga
Bw.Diwani Athumani, diwani huyo alikatwa mapanga Jumamosi iliyopita saa sita usiku nyumbani kwake.

Akielezea tukio hilo kamanda huyo alisema siku hiyo Bw.Kisiminza akiwa nyumbani kwake usku amelala alivamiwa na watu watatu  waliovunja mlango na kuanza kukata mapanga na kuchukua simu yake ya mkononi.

Alisema watu hao baada ya kutoka nyumbani kwa diwani huyo walikwenda kuvamia kwa mwananchi mwingine kijijini hapo Buyange  Bw, Bw.Mussa Robert ambaye naye walimkata mapanga na kuiba simu tano, baiskeli moja na kifaaa kifaa kimoja cha umeme wa sola vyote vikiwa na thamani ya shilingi 567,000.

Kamanda Athumani  alisema baada ya kutoweka watu wa familia hiyo walipiga yowe kuomba msaada ndipo wasamalia wema walipofika na kumchuku yeye na Bw.Robert waliwakimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Segerema
mkoani Mwanza kwa matibabu.

Alisema wakiwa wanatibiwa hapo Bw.Kisiminza alifariki saa nane mchana juzi. Bw. Robart alipata matibabu na kuruhusiwa siku hiyo hiyo kutokana alikuwa na majeraha kidogo.

Kamanda huyo alisema Jeshi la Polisi linendelea na msako na uchunguzi zaidi kusaka watu waliohusika ambapo limetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano ili waliohuika wakamatwe.





2 comments:

  1. Muwe mnaandika na tarehe za habari hizo ili kuleta mhemko zaidi kwani hazionyeshi kuwa ni za lini halafu pia nayi zitawapa nguvu ya kufanya kazi kwani ukijua kuwa kila siku lazima niweke habari mpya. Asante sana kwa gazeti la majira

    ReplyDelete
  2. habari gani hii isiyoeleweka? haina tarehe lilipotokea tukio, habari haieleweki nyie majira vipi? hamna waandishi wazuri? ndiyo maana heshima yenu inakwisha na wtu hawanunui gazeti lenu kwa sababu sasa hili gazeti na wandishi ni wa viti maalum

    ReplyDelete