15 April 2011

Kesi ya kumtishia mke wa Mbowe yaunguruma

Na Angelina Mganga

KESI ya kutishia kuua kwa maneno iliyofunguliwa na mke wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe katika Mahakama ya
Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam, imeanza kuunguruma.

Hakimu Jonas Mahende jana alianza kusikiliza ushahidi wa mlalamikaji dhidi ya mlinzi wa Klabu ya Bilicanas, Bw. Herman John (36) anayedaiwa kutishia kumuua kwa kumtumia ujumbe mfupi wa maneno.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Karani, Bi. Hatanawe Kitogo kuwa Februari 3 mwaka huu, katika club hiyo iliyopo wilayani Ilala, Dar es Salaam, Bw. John alitishia kumuua Lilian.

Bi. Kitogo alidai kuwa, mshtakiwa alituma ujumbe mfupi wa maneno kupitia namba 0762 055605 uliosema kuwa anampa siku saba Lilian amuachishe kazi mtu anayeitwa Power, na kima cha chini cha mshahara wake kiwe 320,000/- la sivyo atakuwa hatarini.

Bi Mbowe aliileza mahakama kuwa mlamikaji alianza kazi ya ulinzi nyumbani kwake Mikocheni mwaka 2009 tangu alipoajiriwa na baadaye kulinda kwenye klabu hiyo.

Bi. Mbowe alieleza kuwa baada ya kupokea ujumbe huo, aliamua kushauriana na mumewe ili amhoji mshtakiwa, lakini mumewe alimwambia akaripoti polisi.

Shahidi namba moja FF 2255 DC Mboka (35) alithibitisha kuwa wakati wa upelezi, mshtakuwa alikutwa na laini mbili za simu na askari alipata uhakika kupitia Vodacom kujua simu iliyotumika kutuma ujumbe huo ni ya mshitakiwa.

Shahidi wa pili Julius Paul (51) ambaye ni Meneja wa Klabu Bilicanas, alimhamisha mshitakiwa kwenda kulinda Mikocheni kwa mama huyo na ndipo alitoa maneno ya vitisho ya kuongezwa mshahara na hadhi kwa wafanyakazi.

Kesi imeahirishwa mpaka Mei 3, mwaka huu ili mshtakiwa aanze kujitetea kutokana na vielelezo vilivyoletwa na mlalamikaji.

19 comments:

  1. umemjibu vizuri sana maana inaonekana jamaaa hana akili kabisa itabidi aende loliondo akatibiwe

    ReplyDelete
  2. Nasikitika sana kwa matusi yaliyokuwa yameandikwa. Kwani ni lazima uchangie matusi yako au unatakiwa utoe maoni yako katika uadilifu kama mtu timamu, ukizingatia watu wa Mungu tunataka tusome na kutoa maoni yetu. Msirudie tena.
    MAONI YANGU.
    Inatakiwa iyo kesi ifanyike kama ilivyopangwa na wengine wajifunze kutokutoa lugha chafu, matusi au kumtishia mtu maisha yake katika simu.

    ReplyDelete
  3. ndugu wasomaji jaribuni kutumia lugha nyepesi kwani mambo kama haya yanayoandikwa yanasomwa na watu wengi kama humekosa kitu cha kukoment ni bora zaidi ukakaa kimya kuliko kutoa matusi ambayo hayana maadili katika nchi yetu magazeti haya yapo kwa ajili kupasha habari watu wote kwa hiyo awawezi kuchagua habari ipi iandikwe ndani ya gazeti.Jaribuni kuwa watu wenye maadili mema matusi sio chanzo cha kumfanya mtu ufahamike na chakushangaza hao waliotoa matusi makubwa kama hayo ni wasomi wazuri ambao wangesaidia nchi yetu katika kuondokana na ujinga lakini wao wamekomalia matusi yani wapendwa inauzunisha sana tena sana

    ReplyDelete
  4. Administrator moderation ya maoni ni muhimu hapa ili kuunusuru uhuru wa kutoa maoni. Wananchi kidogo wamepotoka hapa hasa mchangiaji wa 1:54 hapo juu. Duh, ndugu yetu, hebu kuwa na soni kidogo basi. Gazeti linasomwa na wengi hili.

    ReplyDelete
  5. INATISHA NA KUSIKITISHA, WATANZANIA TUBADILIKE, HEKIMA NA MAADILI NI MUHIMU.

    ReplyDelete
  6. ipotezee haikuhusu hiyo, mbona hujatoa maoni wewe nyie ndo wale wale, jikate jumla yaani kwa sababu hatuwezi kulea usenge kila kona mtokeo yake ndo mafisadi tuliyo nayo kila sekta katika nchi yetu, dawa ni kuwatafuta mmoja mmoja na tnazaa nao. haina noma man pamoja sana mimi ukei kei sipendi hata masela street wananifahamu kabisa. mnaleta ubishi wa kipumbavu kila habari mnajifanya kuichunguza na kujiita wasomi mliojipachika magammba hewa kichwani hamna kitu. unabisha? wewe umesomea nini kama si ujuha tunaendekeza hapa tanzania? bora tungeajiri mzungu awe raisi alafu tumlipe kwa mwezi,

    ReplyDelete
  7. Jamani hata kama kitu hakikufurahishi ni bora ukasema kinachokuuma lakini matusi hayapendezi!! Naungana na mchangiaji wa 2.20 kuwa maoni haya inafaa yachunjwe kwanza ndio yawe published. Tunaomba wahusika wajaribu kuliona hilo!

    ReplyDelete
  8. msiwe na wasiwasi,wavuta bangi ni wengi hapa Tanzania,walishachanganyikiwa na kukata tamaa na maisha.Kwa hiyo lolote analowaza analisema na kuliandika,ni kuchanganyikiwa huko!!! na ndio maana tuna wodi za vichaa!!!!!!! duh,maisha yanachanganya watu si mchezo!! ama kweli kazi ipo kama ndio hivi

    ReplyDelete
  9. Tanzania tumeshakuwa na watu wengi waliochanganyikiwa, hili ni tatizo kwa taifa. wanaoandika matusi hawajielewi, mtatakiwa kuwaombea.
    Hapa kazi ipo,sikutegemea kama nchi yetu ina watu wa aina hii.

    ReplyDelete
  10. WAHARIRI, ndio mnaosababisha matatizo ya matusi yasiyo na msingi; kwa sababu mnashindwa kuhariri habari za kuandika.

    kwa mfano habari ya mke wa mbowe kutishiwa ni habari kweli! lakini yawezekana ingewekwa kwenye ukurasa wa habari za mahakamani, bila kuacha kweka mbele (front page) habari za mikoani za maana ambazo pengine ni nzuri na zimeachwa ambazo wananchi wengine hawazisikii kutokana na kukosa magazeti lakini kwenye radio wangesikia japo kichwa cha habari.
    utawala (Administrator moderation, ufike mahali ufuatilie kazi zenu kwa karibu, ili zisiandikwe kiupendeleo na kwa kuwaangali dar es salaam tu.
    siku hizi mmekazania kuandika habari za kwa njia ya makala huku watu wakilipa 50,000 mwandishi; badala ya wateja kufanya matangazo; matokeo yake habari zinakuwa chache na wanunuzi wanawakimbia.acheni mtindo huo wa kulihujumu gazeti.kama hamlipwi mishahara mgome siyo kulihujumu gazeti.

    ReplyDelete
  11. Daa! Wabongo sasa wengi wamechanganyikiwa na hii ni matunda ya serkali ya CCM kusababisha maisha magumu ndio maana Dr.Slaa alisema ukimuona kijana wa leo kavaa mlegezo usidhani ajaenda shule utakuta huyo ni form four au form six na huku chuoni wanachou wengi inaKaribia nusu ya wanachuo wavulana wanavuta bangi tupige magoti na tusali

    ReplyDelete
  12. Libya serikali imewafanyia kila kitu wananchi lakini leo hawaitaki. Turudi vijjini tukalime.

    ReplyDelete
  13. issa michuzi wa wapi wewe? hili ni gazeti la majira.

    ReplyDelete
  14. hii kesi ya kanga kuileta humu gazetini inahusu nini? mbowe na mkewe wanajitafutia umaarufu tu wa kutaka kuwemo katika kila hadithi kama sungura mjanja. niliipoona "heading"nikavutika kusoma nikadhani labda First Lady kivuli katishiwa na wabaya wao wa CCM kumbe boi wake, aah wakamalizane huko huko! haina tija kwa waTZ

    ReplyDelete
  15. Hii ndiyo picha halisi ya viongozi wajao katika nchi hii,ni viongozi makatili sana,wenye uchu wa madaraka na pesa. HUYU MLALAHOI ATAFIA JELA. NILISHASEMA WAZI KUNA WATU WAMEAJIRIWA KUWA KWENYE INTERNET KUJIBU KILA ISSUE ZA VIONGOZI WA CHADEMA. HUYO HAKUKOSEA KUTAKA MSHAHARA WA 350,000/= KWANI NDIO MAHUBIRI YA CHADEMA KIMA CHA CHINI KUWA HIZO ANAZODAI MLINZI,SASA IWEJE NYIE MNAOHUBIRI MALIPO MAKUBWA KWA WATU WA KIMA CHA CHINI HALAFU NYIE MNAWAPA NDOGO. HATA HUYO MBOWE HANA AKILI WALA BUSARA KUMSHAURI MKEWE AENDE POLISI KWA JAMBO KAMA HILO,ANAYETAKA KUKUUA HUWA HAKUAMBII ANATEKELEZA TU. OLE WENU WATANZANIA NA WATU KAMA HAWA

    ReplyDelete
  16. Kesi ya kipumbafu kabis hii.nyie kina mangi fipi,mbona nyie mmeshaua wengi tu kwa ajili ya pesa,leo huyu katishia tu unataka kumfunga,wewe mbowe ukishika madaraka si utamaliza watu? busara hushinda kila kitu hata majira inashangaza kuipa umaarufu kesi hii ya kijinga

    ReplyDelete
  17. Nilifikiri katishiwa na kigogo wa ccm kumbe upuuzi mtupu

    ReplyDelete
  18. Mhariri tuondolee uchafu huu,mwandishi kahongwa na Mbowe kwa ajili ya kujitangaza

    ReplyDelete
  19. Taratibu, hata kama mtu anatiwa si lazima useme mbona tunajua kuwa wanawake wanatiwa ndo mana wanapata mimba na kuzaa, pia tunajua mashoga watiwa,hivyo basi si lazima kusema, iwapo ni lazima basi tumia istilahi

    ReplyDelete